Uongozi wa Kanisa Katoliki Duniani umesema takriban watu 200,000 wamehudhuria misa ya mazishi ya Papa Francis iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Licha ya uwepo wa marais na wakuu wa nchi, mazishi ya Papa Francis yamehudhuriwa na raia wa kawaida, wafungwa na wahamiaji ambao waliusindikiza mwili wake hadi kwenye Kanisa ambako atazikwa hivi leo.
Kengele za Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro zililia kuashiria mwanzo wa harakati za mazishi ya Papa Francis ambapo uongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Vatican umesema takriban watu 200,000 wamehudhuria misa hiyo ya mazishi inayofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni pamoja na Rais wa Marekani Donald Trumpna mkewe Melania, wa Ufaransa Emmanuel Macron, Volodymyr Zelensky wa Ukraine, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya, Mwanamfalme William wa Uingereza na familia ya Kifalme ya Uhispania na wengineo weng
Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika kwenye barabara kuu inayofahamika kama della Conciliazione ambayo ndio inayoelekea kwenye Uwanja wa Vatican wa Mtakatifu Petro huku wakifuatilia misa kwenye televisheni kubwa zilizowekwa kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Maggiore mjini Roma, ambako Papa Francis P atazikwa baadaye leo Jumamosi na kaburi lake kuandikwa Franciscus.
Waombolezaji wameagizwa kujiepusha na vitendo vya kupeperusha bendera au mabango wakati wa ibada ya misa ya kumuaga Papa Francis.
