Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye moja ya mashine zilizopo katika karakana ya uhunzi na uundaji wa vyuma akipata maelezo kutoka kwa wanafunzi ambao wanajifunza kupata ujuzi wa fani hiyo na kuja kulitumikia taifa hili hata kuanzisha viwanda vidogo vidogo au kwenda kufanya kazi kwenye viwanda mbalimbali
Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akipata maelezo kutoka chumba cha kompyuta ambacho nacho kipo chuoni hapo 
Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye chumba cha mapishi ambako wanafunzi wa fani ya upishi huwa wanajifunza kwa vitendo. 
Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye karakana ya umeme
Hii ni karakana ya useremala ambayo pia inawaongezea ujuzi wanafunzi wa fani hiyo ikiwa na vifaa vya kisasa kabisa
 
 
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kupitia chuo cha ufundi VTC Mdabulo kilichopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa linawasaidia watoto yatima na walio kwenye mazingira magumu kwa kuwapatia elimu ya ufundi bure.
Akizungumza Mkurugenzi mtendaji wa R.D.O Fidelis Filipatali alisema kuwa shirika hilo linawasomesha wanafunzi bure wanatoka katika mazingira magumu na watoto yatima ili kuwapa elimu itakayowakomba katika maisha.
“Lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo mengine kwenye vyuo vingine wanapata nafasi katika chuo chetu hiki ambacho kinagharama nafuu na kinatoa elimu bora ya ufundi ambayo inatamsaidia huko mbele kwenye maisha yake” alisema Filipatali
Filipatali alisema kuwa shirika hilo limebeba dhima ya Rural Devolopment Organization (RDO) kwa kutoa ujuzi endelevu kwa jamii ili kuondokana na kuwa tegemezi katika maisha na kuishi kwa kujitegemea kutokana na ujuzi unaopatikana chuoni hapo.
“Chuo cha ufundi stadi cha RDO VTC na shirika kwa ujumla vinanuia kuinua jamii kutoka a hali ya chini kiuchumi na kufikia hali nzuri ya kimaisha na ndio maana tupo huku vijijini ambako ndio kuna wananchi wengi wa hali hiyo” alisema Filipatali
Lakini Filipatali alisema kuwa chuo hicho kimelenga kuwapa ujuzi wa muda mfupi na muda mrefu kwa lengo la kuwasaidia kuendelea kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.
“Tunatoa ujuzi kwa njia tofauti tofauti hivyo tunapoona kuwa wanafunzi wanauwezo wa kujitegemea na wapo tayari kwenda kujitegemea huwa tunawaruhusu ili kupisha nafasi kwa wanafunzi wengine kupata ujuzi wa kiufundi” alisema Filipatali
Filipatali alisema kuwa wanafunzi wawapo chuoni hapo wanajifunza ufundi bomba,kuchomelea,ufugaji wa ng’ombe,upishi,ushonaji,kilimo,elimu ya kompyuta useremala,ufundi chuma ufundi uashi na ufundi umeme.
“Sasa wanafunzi yeyote Yule akitoka hapa katika chuo chetu anaweza kujitegemea kwa kuwa atakuwa ameshapata ujuzi kwa vitendo anaweza kufanyia kazi mahali popote pale atakapo amua kuweka makzi yake” alisema Filipatali
Aidha Filipatali alisema kuwa vijana wanatakiwa kujituma kwa kufanya kazi na kuacha kuwa tegemezi katika jamii.Naye katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende amewataka wananchi kuwapeleka watoto kupata elimu ya ufundi katika chuo hicho ambacho kinatoa elimu kwa gharama nafuu.
“Haiwezekani kuwa chuo hiki kipo hapa jimboni kwetu lakini wanafunzi wanaosoma hapa wanatoka mbali na kuja kuchukua ujuzi huu wakati sisi wazawa tunawaficha watoto wetu tabia kama hii haikubariki hata kidogo hivyo nawaomba wananchi na viongozi kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu ya ufundi katika chuo hiki” alisema Mdende
Mdende alisema kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo aliwashukuru shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kupitia chuo cha ufundi VTC Mdabulo kwa kutoa elimu bure kwa wanafunzi yatima na wanaishi katika mazingira magumu.