Watoto mapacha wawili Danford Steven Seif (24) na Daniel Steven Seif (24) wanadaiwa kumuua mama yao Upendo Mathew Mayaya (42) kwa sababu ya imani za kishirikina.

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limethibitisha kuwakamata na kuwafikisha mahakamani mapacha hao ambao wote ni wakulima na wakazi wa Mraushi A, Wilaya ya Masasi mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleiman, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

“Watuhumiwa hao walitekeleza kitendo hicho Desemba 15, 2024 kwa kumpiga mama yao katika paji la uso kwa kutumia jembe na mwichi na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo chake” amesema.