Watoto 2,000,000 wanaozaliwa Tanzania 14,000 mpaka 20,000 wanazaliwa na usonji katika kipindi cha mwaka mmoja.

Mkurugenzi Mkuu wa huduma za Kinga Wizara ya Afya, Dk. Hamad Nyembea ametoa takwimu hizo akiwa kwenye usiku wa msimu wa tatu wa harambee wa watu wenye usonji yenye lengo la kukusanya Sh milioni 280 kwa ajili ya mradi wa miaka mitano utakaoitwa ustawi kwa kila mtoto iliyofanyika jana jijini Dar es salaam.

Dk Hamad amesema watoto hao wanaozaliwa wapo wengi kwenye jamii na haijaweza kuwatambua kutokana na kutokuwa na uelewa hivyo serikali inaanzisha huduma za utengamao shuleni na kwenye Wizara ya Afya ni miongoni mwa vipaumbele 10 vya huduma hiyo.

Aidha Hamad amesema kwa sasa wizara hiyo imeanza kufanyia kazi kwa kuongeza viashiria vya kuwabaini watoto wenye usonji kwenye kadi za watoto hivyo wizara hiyo imeanza kufanyia kazi ni kipaumbele chao kwenye magonjwa yasiyoyakuambukiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Lukiza Autism, Hilda Nkabe ameiomba serikali likizo ya ulemavu kwa wamama wanaojifungua watoto wenye ulemavu hivyo kuwe na likizo ndefu ya uzazi na viashiria vya usonji viongezwe kwenye kadi za kliniki za mama na mtoto ili kuweza kutambua watoto wenye usonji au changamoto nyingine kwa wakati.

Awali akizungumza Dk.Edward Kija Mwenyekiti wa Bodi Taasisi ya Lukiza Autism amesema asilimia 80 ya watoto wenye usonji huwa wanachelewa kuongea na wazazi huwa wanaona hivyo mtoto akifikisha miaka mitano mtoto akipelekwa kwenye huduma za utengamao hivyo kuboresha hilo inapaswa wagundulike mapema.Harambee hiyo ilikusanywa kiasi ya Sh milioni 81.6 na bado ni endelevu .