Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Tunduru
Watu watano wamefariki dunia na wengine saba wamenusulika kifo baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kusombwa na maji katika kivuko cha mto Ruvuma kuelekea nchi jirani ya Msumbiji.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari waliofika katika eneo la mto Ruvuma katika vijiji vya Wenje kwa upande wa Tanzania na Lulimile nchi jirani ya Msumbuji.
Akifafanua taarifa hiyo DC Mtatiro amesema kuwa katika tukio hilo mtumbwi huo ulibeba wananchi 12 kwa ajili ya kwenda katika Kijiji jirani Cha upande wa nchi ya msumbuji.
Amesema baada ya tukio hilo lililo tokea February 16 majira ya saa 11 .15 watu wengine ambao hawakuwa na mizigo ya kubeba waliokolewa .
Amesema waliopoteza maishi ni mama mmoja ambaye alikuwa na watoto wake wadogo wawili mapacha wakiwepo wakile na wakiume na mama mwingine ambaye alikuwa na mtoto mdogo pia wakile ndiyo waliozama .
Akizungumzia hatua za uokoaji DC Mtatiro amesema kuwa kwa sasa wazamiaji wa Wilaya ya Tunduru na wengine kutoka mkoani wamefanikiwa kuokoa miwili mmoja wa mtoto na badi wanaendelea na mapambano ya kuisaka miili minne iliyobakia.
Kufuatia tukio hilo DC Mtatiro amepiga marufuku uvushaji wa watu katika eneo hilo hasa kipindi hiki ambacho mto Ruvuma umefirika maji na kwamba ikitokea wanavuba basi wawe watu wazima wanaume ambao wanaweza kuogelea endapo itatokea zoruba yoyote.
Aidha katika taarifa hiyo DC Mtatiro pia ameahidi kutoa taarifa ya maendeleo ya uokoaji February 18 majira ya jioni namna zowezi la ukowaji wa miwili hiyo linavyo endelea
“Namwakikishia Mkuu wa Mkoa wa Katavi na wananchi wa kijiji cha Katambike na Kata ya Ugalla kwamba mradi huo utakamilika ndani ya mwenzi ujao wa tatu na wananchi wote watapata huduma ya maji.Sasa tunachofanya kampuni ipo kazini na mimi sitaondoka na sijaondoka mkoani Katavi hadi mradi huu ukamilike” Alisema.
Katika hatua nyingine alimpongeza Mkuu wa Mkoa kwa kazi nzuri ya kufuatilia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) wa ujenzi wa miradi katika mkoa wake kwa kuwa ni wajibu wake na anaifanya kazi hiyo kwa ukaribu sana.
“Nichukue fura hii kumshukuru rais Dk Samia Suluhu Hassain kwa kazi nzuri ya kumwaga miradi mingi kwenye nchi nzima na kutupatia fursa nzuri wakandarasi kuweza kutumia fursa hiyo na serikali kuendelea kuwaamini wakandarasi wa ndani” Alisema Dunga.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko anaendelea na ziara yake katika mkoa huo ambapo amekuwa akikagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoa huo na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.