WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amewataka Watanzania kupuuza maneno ya wa wanasiasa wanaopita maeneo mbalimbali nchini na kueneza habari za uchochezi kuhusu Uchaguzi Mkuu.
Ndumbaro amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza sababu zinazoweza kusababisha Mtanzania kutoshiriki uchaguzi na imebainisha uchaguzi kama haki ya msingi ya kila mwananchi wenyewe umri wa kuanzia miaka 18.
Ndumbaro amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kampeini ya kisheria katika Mkoa wa Kagera iliyofanyika katika viwanja ya Mayunga vilivyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambapo mamia ya wananchi wamejitokeza kuleta changamotoo zao za kisheria na kuziwasilisha kwa wanasheria na wengine kupata fursa ya kukabidhiwa mawakili mbele ya waziri huyo.
Kupitia kampeini hiyo amewahakikishia wakazi wa Kagera kuwa kampeni hiyo ni endelevu na tayari wizara imewaajili maofisa dawati wa kushughulikia malalamiko ya kisheria wilayani wapatao 400 nchi nzima huku wanasheria wasaidiz walipewa mafunzo kwa ajili ya kutoa huduma za kisheria wamefikia 2,500.
“Wananchi msiwe na wasiwasi tumeshuhudia mafanikio makubwa sana kupitia kampeini ya mama Samia ya msaada wa kisheria na toka kampein hii ianzishwe mwaka 2023 asasi za kiraia zinazotoa huduma za kisheria zimeongezeka kutoka 85 hadi 387″alisema Ndumbaro.
Alitoa wito kwa viongozi wa dini kutoacha kukemea wananchi wanaojichukulia Sheria mkononi, kwani wanageuka chanzo cha mitafaruku na migogoro iisyohisha ,pia amezitaka familia kutafuta soluhisho la kupatana kwani familia nyingi ndizo chimbuko la migogoro ya ardhi na miradhi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa alisema kuwa mkoa huo utawavua mamlaka wenyeviti wa vijiji na mitaa pamoja na kuwatengua watendaji wa mitaa na vijiji wanaosabanisha migogoro ya ardhi kwani wao wamekuwa chanzo cha migogoro ya ardhi mara kwa mara.
“Mkoa wa Kagera huu hata vitendo vya mauaji mara nyingi vinasababishwa na migogoro ya ardhi ,mara nyingi wenyeviti wa vijiji wanauza maeneo ya wananchi migogoro haiishi na hapohapo tunapata watu wanalipiza visasi ,sasa kama mkoa tunapanga kuchukua hatua madhubuti ,kuwawajibish,” alisema Mwassa.

