Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kilimanjaro
Kuekelea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, Wananchi Wilayani Same Mkoni Kilimanjaro wametakiwa kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo kwenye maboksi ya kura pamoja na kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi ili kiendelee kuwaletea maendeleo wananchi kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya Same Kasilda Mgeni wakati akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara eneo la Stendi ya Mabasi ya Same mjini, wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero na malalamiko mbali mbali ya wananchi Pamoja kuwaeleza dhamira ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samaia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Same ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Vile vile sisi kama viongozi wa Serikali tuliopewa dhamana ya kumuwakilisha kwenye maeneo haya tutaendelea kutatua kero na malalmiko yanayowakabili wananchi wetu kwa kufanya mikutano ya hadhara kwenye maeneo yenu na tutaendele kuwajibika kwa vitendo ili wananchi wetu muweze kuishi kwa usalama na amani kwenye Wilaya yetu ya Same”.