Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar e Salaam

Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na Jinsia na Mabadiliko ya Tabia nchi, (Wated) limewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelimisha jamii kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na mazingira yanayoendelea katika maeneo ya mbalimbali na namna ya kukabiliana nayo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku mbili, yaliyowashirikisha wadau mbalimbali wa kilimo, mifugo, na wanahabari, yaliyofanyika jijini.

Mratibu wa shirika hilo Maria Matui , amesema lengo la kuwakutanisha
Waandishi wa Habari pamoja na wadau wa kilimo na mifugo kutoka katika mikoa mbalimbali kujadili kwa pamoja masuala yanayohusu mabadiliko ya tabia nchi na mazingira.

Maria amesema wame vishirikisha vyombo vya Habari, kwasabau ndiyo vinaweza kufikisha ujumbe kwa watunga sera na kuona ni jinsi gani jamii inakabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi hususani wanawake na Watoto kwani ndiyo waathirika wakubwa.

Amedai hadithi zao, zinaweza kusika mbali zaidi na kuleta uchechemuzi wa utekelezaji wa sera ,kanuni na sheria .

Amesema wadau walio kutana wanahusika katika mradi unaolenga masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na mazingira.

“Mradi huu umefika Karagwe, Ngara, Mafia lindi, Mtwara, na Dar es Salaam.

Lengo kuu ni kuchunguza jinsi gani Wanawake na Wasichana
wanavyoathirika moja kwa moja na mabadiliko ya tabia nchi na jinsi
wanavyoweza kuhimili kupita miongozo, kanuni, sheria, sera.

Tumeandaa mafunzo haya, kwa sababu tulifanya mradi katika maeneo haya
na tulikuta kuna changamoto za tabia nchi na mazingira ndiyo maana tumekutanisha wadau hawa wapate fursa ya kuelezea baadhi ya masuala yanayohusu mabadiliko ya tabia nchi.

lakini swali ni jinsi gani wanavyo himili mabadiliko haya. pia, ni heria na kanuni zipi zinazo waongoza katika kukabiliana na hali hiyo hasa katika mambo ya rasilimali fedha, haki, na wajibu.

Tumeona katika siku hizi za karibuni Mafia jinsi gani waliathirika na masuala ya mafuriko ,Kagera ni jinsi gani walikumbana na ugonjwa wa mnyauko.

Pia wameangalia jamii za Wafugaji wilaya kiteto, jinsi gani mila na desturi zimemweka Mwanamke wa Kimasai nyuma na jinsi wanavyo kabiliana na mabadiliko ya tabia nchi” Amesema.

Dkt Gradness Munuo mwandishi wa habari mkongwe na mratibu wa kituo cha
msaada wa kisheria (CRC) amesema mafunzo yamejikita katika kujadili
mabadiliko ya tabia nchi na umuhimu wake kwa wanahabari katika kusambaza taarifa.

Amesema wanahabari wanapaswa kuelewa kuwa wao ni kioo cha jamii, hivyo ni muhimu pia kufahamu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na mazingira, ambayo yanaathiri jamii kwa ujumla.

Aidha, waandishi wa habari wanahitaji sana kuelewa masuala ya kijinsia na jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri hali hiyo.

“Tunatambua kuwa mabadiliko ya tabia nchi na mazingira yanamgusa mwanamke kwa kiwango kikubwa, kwani yeye ndiye anayeshughulika kwa kiasi kikubwa na shughuli za kilimo, kutafuta maji, na nishati ya kupikia chakula.

Waandishi wanaweza kutumia kalamu zao, kumwelewesha mwanake kuhusu
madhara ya kupikia kuni mbichi, kwasababu anatumia muda mrefu kuhakikisha inawaka wakati angefanya vitu vingine.

tunajua waandishi wanajua changamoto, zinazowakabili wanawake katika mabadiliko ya tabia nchi kuhusu suala zima la nishati ya kupikia kwa hiyo kama anahabari, mnapaswa kupaza sauti zenu kwa watunga sera

Nishati safi tunayo hitaji Mwanamke wa Kitanzania, aweze kuitumia kwa
urahisi inapaswa kupatikana kwa bei inayoweza kumudu, ili hata
Wanawake wa kijijini wapate fursa ya kuitumia, hasa Mamalishe na katika majumba, magereza na Mashule.

Hii ni kazi ya upatikanaji wa Nishati iwe rafiki kwa wote, wana habari wanahitajika kusimamia kilio cha wanawake.

Mimi naweza kusema nina uwezo wa kununua , sasa ambaye kipato chake
ni kidogo anaweza kufikia hili tunapaswa kulipazia sauti.

Serikali yetu, chini ya uongozi wa Mama Samia, imefanya juhudi kubwa
kuhakikisha kuna maboresho katika mazingira ya kilimo na maji.

Ingawa mvua hazinyeshi kama ilivyotarajiwa, ni muhimu kutafakari chanzo cha tatizo hili, ambalo linaweza kuwa ni ukataji wa miti au mabadiliko ya tabia nchi.

Katika kutatua changamoto hii, ni muhimu kuwashirikisha viongozi wa kimila na dini ili kufikia malengo yetu, na hapa wanahabari wana jukumu muhimu ili kufanikisha hili

Jane Atanasi kutoka Ngara, mimi nipo hapa kuwakilisha Wanawake walioko kule kwetu, mafunzo haya imeweza kutufundisha mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi na mazingira.

Ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiri sana maisha yetu, kwani hapo awali tulikuwa na aina mbili za ya chakula na pombe ilitumika kibiashara kwenye kuapata mapato ya kujenga Nyumba na kupeleka watoto shule.

“Hata hivyo, baada ya mabadiliko ya tabia nchi, mkoa wetu umekumbwa na
ugonjwa wa Mnyauko, ambao umekuwa na changamoto kubwa kwetu. Tumefanya
juhudi mbalimbali, ili kukabiliana nao lakini tumeshindwa pamoja na kushirikiana na Serikali.

Kwa sasa tumehamia kwenye kilimo cha mahindi ,mpunga na vingine ,kwa hiyo tunaomba msaada wa Serikali tupate mashine au kuchimba visima kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji amesema.

Aisha Hafsa anatokea Chole, Mafia amesema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sana maisha yao hadi kufikia hatua ya kupoteza mali, majumba, na mazao walipo kumbana na mafuriko.

“Tangu tulipokumbana na matatizo haya, tumefanya juhudi tena mwezi huu, na tunaomba Mungu atujalie kupata msaada kutoka kwa serikali kwa ajili ya vikundi vya wakulima.

Pia, nimenufaika na elimu kuhusu afya ya akili, ambayo imenisaidia kuelewa kuwa baadhi ya watu tunaowaona wanaweza kuwa na matatizo ya akili.

Mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha ukame mkubwa katika eneo letu, na mimea imekufa kutokana na jua kali na ukame.

Paulina Lendwe amesema wao kama jamii ya wanawake wafugaji, wanakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na jukumu lao la kuhakikisha nyumba zao zinakuwa na maji muda wote .

Amesema mara nyingi, wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji,
jambo ambalo si rahisi, hasa kwa sababu waume zetu hawajihusishi na kazi hii.

“Wakati wa ukame , hali inakuwa mbaya zaidi kwetu , visima vinakauka na Ng’ombe wanahitaji maji.

Kama wanawake, tunapaswa kuhakikisha kuwa nyumba zetu zina maji, hata wakati tunapokuwa na changamoto kama za kujifungua, tunapaswa kufanya hivyo labda tunapata msaada kutoka kwa wanawake wenzetu.

“Hata hivyo, tunashukuru shirika la Wated kwa kutufundisha jinsi ya kujitegemea.

Nilikuwa katika hali ngumu ya kuishi kama mke, lakini kupitia mafunz ya WATED nimeweza kujifunza jinsi ya kujitegemea Amesema.

Katika mafunzo hayo, washiriki walipata fursa ya kujifunza kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na mazingira.

Pia, walijadili changamoto mbalimbali zinazo husiana na mabadiliko ya tabia nchi, kulingana na mazingira yao na mikakati wanayotumia kukabiliana nazo.

Mafunzo hayo yalilenga kuwapa uelewa wadau wa sekta hizo kuhusu jinsi
ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.