Na Happy Lazaro, JamhuriMedia, Arusha

Chama cha Wataalamu Watoa Dawa za Usingizi na Ganzi Tiba Tanzania ( TANPA) kimekutana mkoani Arusha kwa lengo la kujadili namna ya kuondoa changamoto zilizopo kwa wataalamu hao na kuweza kuboresha utoaji wa huduma  katika idara hiyo. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la  3 la kisayansi la wataalamu hao  linalofanyika jijini Arusha kwa siku tatu,amesema kuwa lengo la kongamano  hilo ni kuweza kubadilishana mawazo na uzoefu na kuweza kupata uelewa zaidi katika maswala hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya tiba ,mifupa na ubongo kutoka Muhimbili na Mlezi wa chama hicho Dkt Mpoki Ulusubisya akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano hilo jijini Arusha .

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya tiba na mifupa na ubongo kutoka Muhimbili na Mlezi wa chama hicho Dkt Mpoki Ulusubisya  amesema ni wakati wa kubuni mbinu mbadala katika Afua za utoaji huduma na kupunguza vifo vya watoto wachanga huku asilimia 6 ikihusishwa na utoaji wa dawa za usingizi huku kukiwa na vitendekazi  hafifu .

Kwa upande wake Rais wa Chama cha wataalamu watoa dawa za usingizi na Ganzi Tiba  Tanzania ,Julia Mahemba  amesema kongamano hilo la  3 linalofanyika kila mwaka  limejumuisha madaktari wa usingizi, matabibu ,wauguzi na wakunga kutoka Tanzania bara na visiwani kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma bora ,salama za upasuaji na kutathmini utendaji kazi wao.

“kupitia kongamano hilo wataweza kutambua pia nafasi yao katika utoaji wa huduma hiyo kwani ni sekta muhimu sana nchini .”amesema Mahimba .

Aidha ametaja changamoto iliyopo ni uwepo wa wataalamu.wachache katika maeneo ya utoaji wa huduma ya afya jambo ambalo.linafanya kazi hiyo kutofanyika vizuri.

Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo  Daktari bingwa Venance Misago na Samweli Mushi amesema kuwa,kupitia kongamano wataweza kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wao wa kila siku na kuweza kuokoa afya ya Mama na mtoto.

Rais wa Chama cha wataalamu watoa dawa za usingizi na Ganzi Tiba Tanzania ,Julia Mahemba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo

Wamesema kuwa,wameweza kupata ujuzi wa kutosha katika kuhudumia.wakina mama wajawazito ambapo wameahidi kuendelea kujiendeleza kimasomo zaidi kwani uhitaji bado ni mkubwa .

Dokta Mushi amesema kuwa, kuna haja ya kuongeza wataalamu  hao kwani uhitaji bado ni mkubwa sana na kila mmoja anajua upasuaji hauwezi kufanyika bila kupewa dawa hizo hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kuongeza wataalamu hao.