Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, kesho ataanza ziara ya kikazi mkoani Dodoma kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kuimarisha chama.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma leo April 22, 2025, kupitia ziara hiyo Wasira atazungumza na wana CCM na wananchi katika matukio na shughuli mbalimbali.
Taarifa hiyo inasema kuwa, katika ziara hiyo ya siku tano, Wasira atatembelea wilaya zote za mkoa huo, ambapo pamoja na mengine ataweka mawe ya msingi kwa baadhi ya miradi ya maendeleo.
“Wanachama, wapenzi wa CCM na wananchi wote wanaombwa kujitokeza kwa wingi kumlaki Makamu Mwenyekiti Wasira katika maeneo mbalimbali atakayoyafikia kupitia ziara hii,” inaeleza taarifa hiyo.
