Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza, wamekutana na kuzungumza wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera.

Wasira na Dk. Bagonza wamekutana jana wilayani Ngara, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara mkoani Kagera.