Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es Salaam
Mkutano wa Mafunzo wa Jumuiya ya askari Polisi wa Kike wa Duniani Ukanda wa Afrika (IAWP – International Association of Women Police – African Chapter) utafungua milango ya mashirikiano katika kupambana na uhalifu unaovuka mipaka na kujenga mahusiano mazuri na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Akiongea wakati wa mafunzo hayo leo Julai 24,20223 Kamshna wa Jeshi la Polisi Zimbabwe Grace Ndou amebainisha kuwa wameanza kujengewa uwezo kutokana na mada mbalimbali zilizotolewa kwa washiriki na wawezeshaji wa fani mbalimbali.
Ameongeza kuwa leo wameanza vizuri mafunzo kupata mada zinazo husiana na Uongozi na Usimamizi wa Kimkakati na Mawasiliano ya Kimkakati ambayo amebainisha kuwa yatawasaidia katika utendaji wa kazi za Polisi.
Kwa upande wake mshiriki kutoka Tanzania mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Gorgina Matagi amesema kuwa mafunzo hayo kwa siku ya leo yamewajengea ufahamu zaidi katika maswala ya ukatili wa kijinsia,rushwa na namna ya kufanya kazi na jamii.
Pia Sajenti wa Polisi Mwanema Salehe kutoka Arusha amebainisha kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati mwafaka kwani tumejifunza kutoka kwa wageni na wao wamejifunza kutoka kwetu.Ameongeza kuwa wamejifunza namna ya kuishi na jamii.