Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,

Benki ya CRDB imewapata washindi sita wa awamu ya kwanza wa kampeni ya ‘Tembo Card Shwaa’ ambao wamejishindia safari ya kutalii mbuga ya Serengeti wakiwa na wenza wao.

Kampeni hiyo ilizinduliwa Februari 13, mwaka huu, huku ikirajiwa kufika tamati Juni mwaka huu ambapo itakuwa na washindi wa awamu nyingine mbili ikiwemo ya mshidi kinara wa kampeni hiyo ambaye atajishindia gari jipya.

Katika droo ya kuwapata washindi hao sita Meneja Mwandamizi Kitengo cha Kadi Benki ya CRDB, Karington Chahe amesema siri ya kuwa mshindi ni kuchanja na Tembo Kadi Mshua katika kila matumizi.

“Kampeni hii inalenga kukuza matuzmizi ya kadi zetu pendwa zenye brand kubwa ya Tembo Kadi, na inakuja na zawadi kabambe, zawadi ya kwanza ni kupeleka washindi 24 mbuga ya Serengeti kwa ajili ya kwenda kushuhudia mambo mbalimbali yanayofanyika ndani ya mbuga ya Serengeti. Lakini pia kuendeleza ile kauli mbiu yetu ya royal tour.

“Leo tumefanya droo ya kuwapata washindi wetu wa Serengeti awamu ya kwanza ambao ni washindi sita, lakini ikumbukwe wakati wa uzinduzi wa kampeni hii ulikuwa wakati wa Valentine kwaiyo ilikuja na mahadhi ya ki valentine kwa hiyo washindi hawa sita tuliowapata tutawapeleka Serengeti wakiwa na wapendwa wao yaani kitaalamu tunaita mshindi na mwenza wake.” Amesema na kuongeza kuwa.

“Kumbuka nimesema Serengeti tumepanga kupeleka washindi 24 yaani washindi 12 pamoja na wenza wao wanakuwa 24. Leo tumepata washindi sita kila mmoja akija na mwenza wake maana yake wanakuwa 12 ambao tutawapeleka Serengeti.

“Lakini kampeni hii ina zawadi nyingi, zawadi ya Serengeti ni zawadi moja katika zawadi nyingi ambazo zimesheheni kwenye kampeni hii. Awamu ya pili ya kampeni hii tutakuwa na washindi watano ambao hao tutawapeleka Ulaya. Tunasema Tembo Kadi Shwaa kiulaya ulaya ambapo watalipiwa kila kitu na Benki ya CRDB na watatembelea zaidi ya nchi tano za Ulaya.” amesema Chahe na kuongeza kuwa.

“Siri ya kuwa mshindi ni rahisi sana tumia Tembo Kadi yako unapofanya miamala yote ya malipo, lakini isitoshe kampeni hii ina zawadi kubwa zaidi, mshindi wa jumla wa kampeni hii ambayo itaisha mwezi wa sita ataondoka na agari aina ya Ford Ranger mpya ziro kilometa.

“Siri ya ushindi ni ileile tumia Tembo kadi yako kufanya miamala unapokuwa dukani tumia kadi yako, super market tumia kadi yako, unanunua tiketi online tumia kadi yako, nje ya nchi tumia kadi yako, jinsi unavyozidi kutumia kadi yako ndivyo unaongeza nafasi ya kushinda kwenye zawadi hizi.

“Na kuonyesha kwamba kampeni zetu ni halisia leo tumefanya tukiwa mubashara kuwapata washindi sita, watanzania ambao wamekuwa wakitufuatilia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii wameona namna washindi wetu wanavyopatikana.

Mwisho amewaasa watanzania “Nitoe rai kwa watanzania wahakikishe wanafungua akaunti za CRDB na wanapata kadi za Tembo kuwa sehemu ya fursa mbalimbali ambazo CRDB imekuwa ikizitoa.”