Polisi nchini Ujerumani imefanya msako katika majengo kadhaa kusini magharibi mwa nchi hiyo ili kuwakamata watu wanaojihusisha na usafirishaji haramu wa binadamu .
Jeshi la Polisi nchini humo tayari limeshapokea hati nne za kuwakamata na msako huo utaendelea kufanyika katika nyumba 24 katika miji ya Mannheim, Karlsruhe na Worms.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi imesema watu hao wanaosafirishwa wanatokea Mashariki ya Kati na eneo la Caucasus ambapo wakiingia wanapatiwa kazi za kufanya bila vibali vya makazi.
Mpaka sasa kundi la watu saba wameshakamatwa na wanaendelea kuchunguzwa huku polisi ikiendelea kuwafuatilia wengine wanaotuhumiwa kuhusika na usafirishaji wa watu na kuajiri wahamiaji bila vibali vya makazi.