Na Mussa Augustine,JamhuriMedia,Dar

Wananchi wameaswa kuwa na utamaduni wa kuokota taka kwenye maeneo yanayowazunguka na kuzihifafhi sehemu salama ili kusaidia kuepukana na magonjwa ya mlipuko yatokanayo na Uchaguzi wa mazingira.

Hayo yamesemwa leo Novemba 2 ,2022 na Afisa Tarafa ya Kariakoo Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam Christina Kalekezi wakati wa uzinduzi wa mpango wa Siku ya Waokota taka Duniani iliyofanyika Jijini Dar es Salaam ,ambapo amesema kuwa bado jamii inatambua kuwa kazi ya kuokota taka ni ya kikundi maalumu ama watu wasio na ajira na hata watu wasio na akili timamu lakini ni wajibu wa kila Mtanzania.

Afisa Tarafa Kariakoo Christina Kalekezi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Siku ya Waokota Taka Jijini Dar es Salaam.

Aidha afisa tarafa huyo ambaye alizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzi Ludigija kwenye Uzinduzi wa mpango wa siku ya Wakusanya taka Duniani,nakusisitiza kuwa kuwa Jamii ndio inatupa taka hovyo, hivyo inapswa kuendelea kupewa Elimu ya kukusanya nakuzihifadhi sehemu salama.

“Shughuli ya ukusanyaji taka ni ya Serikali lakini nyinyi wakusanya taka hamlali ,mnaisadia Serikali kukusanya taka hizo,kwa kweli serikali inatambua mchango wenu wa kuweka mazingira safi,

“Taka zinazozalishwa ni ajira,pamoja na nyinyi kufanya mazingira kuwa safi lakini mnachangia kwa kiasi kikubwa usalama wa afya kwa wananchi na kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita ya kuweka mazingira safi na salama,kwani bila afya njema Taifa haliwezi kuwa na Maendeleo,” amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taka ni Ajira, Alen Kimambo( katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya “Taka Ni Ajira Foundation” Alen Kimambo amesema kwamba siku ya waokota taka Duniani imezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ikiwa na dhumuni la kutambua kazi ambazo waokota taka wanazifanya katika mazingira magumu na hatarishi nakuwafanya wawe kitu kimoja katika kupaza sauti zao kwa wadau wa Uzalishaji wa taka na serikali kwa ujumla.

“Malengo ya serikali ya kufukia taka ziro hayawezi kufikiwa bila kuwatambua waokota taka ambao wanafanya kazi kwenye maeneo ya mitaani na sehemu zingine,hivyo sisi kama Taka Ni Ajira Foundation na Washirika wetu Nipe Fagio tunajaribu kutengeneza msingi wakiwa na sauti ya pamoja na sio mtu mmoja mmoja” amesema Kimambo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Nipe Fagio Anna Rocha( katikati)

Naye Mkurugenzi wa Nipe Fagio Anna Rocha amesema kwamba asilimia 60 ya taka zinazopelekwa kurejerezwa zinapitia kwa waokota taka ,hivyo mwaka 2019 taasisi hiyo ilianzisha kampeni yakuwafanya waokota taka ( Waste pickers) watambulike akitolea mfano kikundi cha Wakusanya taka waliopo Bonyokwa kata ya Tabata Segerea

Hata hivyo mwenyekiti wa kikundi cha wa waokota taka Bonyokwa John Yusuph, amesema kuwa kipindi akiaza kufanya kazi hiyo alidhalauliwa na Jamii, nakuonekana hafai na hana thamani ,nakwamba inapotokea vitu vinaibiwa lawama zinapelekwa kwa Waokota taka,hivyo ameiomba halmashauri ya Ilala iwapatie vitambulisho ili wafanye kazi bila usumbufu.

Halikadhalika baadhi ya waokota taka wameiomba Serikali kuwaondolea changamoto zinazowakabili ikiwemo vifaa vya kinga ,mikopo ya halmashauri,kutambulika na kupatiwa vitambulisho,huduma ya bima ya afya pamoja na fidia kutoka kwa makampuni yanayozalisha taka.