Chama cha mchezo wa kuogelea kwa waogeleaji wenye mahitaji maalumu (Tanzania Para Swimming Association/ TPSA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanategemea kuendesha mashindano ya pili ya kitaifa ya kuibua vipaji vya waogeleaji wenye mahitaji maalumu.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika jumamosi ya wiki, oktoba 12 mwaka katika bwawa la kuogelea la Shabaan Robert lililoko Upanga , Dar es salaam.
Mashindano hayo ya kuogelea yanahusisha waogeleaji wenye changamoto mbalimbali ikiwemo ulemavu wa viungo, ngozi, macho pamoja na usonji ambao wataonesha vipaji vyao vya kuogelea wakishindana kutokana na umri wao na aina ya ulemavu wao.
Akizungumza mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo Bi: Thauriya Diria amesema kuwa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo inafanya kila juhudi kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa mafanikio makubwa na kwa muendelezo wa kila mwaka na kuongeza kuwa waogeleaji watakao vizuri watachaguliwa kwenye timu ya taifa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo zaidi na kuweza kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.
“Tumejiandaa kuona mashindano haya yanafanyika kwa mafanikio huku tukitarajia kuona wachezaji watakaofanya vizuri watapatiwa mafunzo zaidi na kuweza kushiriki mashindano kadhaa ya kimataifa.”
“Kubwa wachezaji hao tunawatafutia wapate leseni na kupatiwa daraja kutoka kwa chama cha kuogelea cha dunia.” Amesema.
Aidha mashindano hayo yataenda sambamba na zoezi la upimaji afya ambapo huduma hiyo itaendeshwa bila malipo yoyote na wataalamu waliobobea kutoka hospital Tiba.