Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Morogoro

Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari dogo walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Kwambe Point A Dumila, wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Marwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ajali hiyo iliyotokea leo Januari 14,2023 ,saa mbili asubuhi maeneo ya Kwembe barabara kuu ya Dodoma- Morogoro ikihusisha gari dogo aina ya Spacial yenye namba T 162 DGM ikitokea Dodoma kuelekea Dara es Salaam iligongana na gari T 654 DDN ikiwa na tela namba T 418 DDP ikitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Amewataja waliofariki ni Samil Ally (26), mkazi wa Mbezi, Forstina Macha Paula Macha mtumishi wa Kanisa, Rahma Said mtoto mwenye miaka 8 aliyekuwa anasoma darasa la nne na Sumay Said mtoto wa miezi 9, wote wakiwa wamehifadhiwa katika Hospital ya St. Joseph iliyo Dumila wilayani Kilosa.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo aina ya Spacial kutaka pita gari la mbele na kugongana uso kwa uso na lori hilo.