Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola wanatarajiwa kufanya kikao maalum kujadili jinsi ya kufadhili utafiti na matibabu ya ugonjwa wa malaria.Haya yanajiri wakati wanasayansi duniani wakiendelea na kikao cha kujadili hatua dhidi ya Malaria Dakar,Senegal.
Huko Kenya wanasayansi kutoka Chuo cha Utabibu cha Liverpool School of Tropical Medicine- Uingereza ,pamoja na taasisi ya utafiti wa dawa nchini KEMRI wamefanya utafiti na kugundua dawa inayoangamiza mbu anayesababisha Malaria. Ng’endo Angela alikuwa Kisumu Magharibi mwa Kenya ambapo kuna visa vingi zaidi vya ugonjwa wa Malaria, na kuandaa taarifa hii..