Kenya imekosolewa na Shirika la Kudhibiti matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli kwa kukosa kufanya uchunguzi katika ongezeko la visa vya wakimbiaji wa Kenya wanaoshukiwa kutumia dawa hizo.

Tangu mwaka wa 2012 wakimbiaji 17 wamesimamishwa kwa muda kutoshiriki mashindano ya Kimataifa kwa madai ya matumizi ya dawa hizo za kusisimua misuli, ikilinganishwa na wawaili kati ya mwaka wa 2010 na 2011.

 

Shutuma hizo zitazungumzwa katika kongamano la shirikisho la kukabiliana na matumizi ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli katika michezo huko Johannesburg Afrika Kusini, mwezi ujao

 

Hata hivyo ni jukumu la baraza la kimataifa la michezo ya Olimpiki ni kuamua kama wachezaji wanaweza kusimamishwa kushiriki katika mashindano ya riadha kwa siku zijazo. “Ikilinganishwa na nchi nyingine, tatizo la Kenya si kubwa zaidi” anasema Mwenyekiti wa wanariadha wa Kenya, Isaiah Kiplagat.

 

Vikwazo hizo vinaonekana kutotekelezwa kwa sasa, lakini Mkurugenzi wa Shirikisho la Kukabiliana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli, David Howman ameuudhika kwa sababu Kenya haijachukua hatua zozote tangu madai hayo kutolewa.

 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa wanariadha wa Kenya Isaiah Kiplagat na Wizara ya Michezo, shirikisho hilo liliwapa fursa hadi Novemba mwaka huu kutoa ripoti kuhusu hatua walizochukua.

 

BBC