Wanachama wanane wa Chama cha ACT- Wazalendo wamechukua fomu kugombea ubunge wa jimbo la Wete lililopo Pemba Visiwani Zanzibar.

Miongoni mwao ni mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Omar Ali Omar, Makamu Mwenyekiti wa Vijana Taifa Nassor Ahmed Marhun, Katibu wa Mkoa wa Wete Masoud Juma Mohamed, Mbarouk Salim Ali (Mbunge wa zamani), Ahmed Suleiman Ali (Mwenyekiti wa Vijana Jimbo la Wete), Farid Juma Sharif (Mjumbe wa Kamati ya Uongozi Tawi la Bopwe), Ali Hassan Dhaty na Rashid Muhammed Abdullah ambao ni wanachama.

Wete, Jimbo ambalo ACT Wazalendo inaliongoza inatarajiwa kuvutia wagombea zaidi na kuufanya mchakato wa kugombea ubunge jimboni hapo kuwa mkali zaidi.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ado Shaibu zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea jbunge ndani ya ACT Wazalendo linaendelea hadi Mei 31, 2025.