Na Zulfa Mfinanga, JamhuriMedia Arusha

Wananchi zaidi ya elfu moja wamefikiwa na kampeni ya Samia Legal Aid iliyoanza March 1 mwaka huu Jijini Arusha huku idadi kubwa ikitajwa kuwa ni wanaume.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kampeni hiyo Ester Msambazi amesema wananchi 1,844 wamefikiwa huku wengi wakiwa ni wanaume kwani wao hubeba changamoto nyingi kwenye familia.

Mkurugenzi wa Kampeni ya Samia Legal Aid Ester Msambazi.

Amesema wamepokea migogori 677 huku migogoro 136 ikiwa imetatuliwa na tayari wameshaandikiwa makubalinao kwa ajili ya kuyawasilisha mahakamani kwa wale ambao migogoro yao ipo katika ngazi ya Mahakama.

“Migogoro ya madai ndo inaongoza Arusha, lakini hadi sasa tumefanya kazi kubwa na lengo la serikali limetimia…..pia kwa migogoro ambayo mashauri yake yapo mahakamani itaendelea kufuatiliwa na kuwasilishwa kadri ilivyofikishwa” amesema Msambazi.

Amesema baada ya kumaliza zoezi hilo mjini Arusha wataelekea wilayani kama ambavyo Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro alivyoagiza ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msambazi, wananchi kutoka wilaya zote za mkoa wa Arusha pamoja na mikoa jirani wamefika na kuhudumiwa.

Hadi kufikia mwezi February 25 mwaka huu tayari mikoa 22 imefikiwa na kampeni hiyo.

Rais wa TLS Wakili Boniface Mwabukusi akitoa msaada wa kisheria kwa mwananchi.