Nesi kutoka Mpango wa  Taifa ya Benki wa damu salama Catherine Kiure akimuhudia moja ya wahamasishaji wa uchangiaji damu Prosper Magali wakati wa uchangiaji damu unaoendelea katika Enep la Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa wamejitokeza kuchangia damu salama uliohamashihswa na Prosper Magali kwa ajili ya kuhakikisha bnki ya damu inakuwa na damu ya kutosha.
Mwandishi wa MMG/Kajunason Blog Cuthbert Kajuna akiwa anachangia damu leo Jijini Dar es salaam.
Mwandishi na mshereheshaji maaruf nchini Taji Liundi ‘Master T’ akiwa anachukuliwa vipimo kwa ajili ya kuchangia damu  katika benki ya taifa ya damu salama nchini uliohamishwa na Prosper Magali.
Muhamasishaji Prosper Magali akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kilichompelekea kuamua kuhamasisha uchangiaji wa damu baada ya kutokea kwa ajali ya dada yake na kupelekea kuhitajika kwa damu haraka sana na kuoma kuna ulazima wa kuhamasisha wananchi waweze kuwa na utamaduni wa kuchangia damu.
Dkt Avelina Mgesa ambaye ji Meneja Damu salama kanda ya Mashariki akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kufurahishwa na hatua aliyoamua Prosper Magali ya kuamua kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa ajili ya kuhakikisha matarajio ya kufikisha malengo ya lita 450,000 za mahitaji ya damu kwa mwaka.

Kutokana na ukosefu wa damu katika benki ya damu salama, Prosper Magali ameamua kuhamasisha watanzania kuchangia damu kwa ajili ya kufikia malengo ya benki ya damu kwa mwaka.

Magali amefikia hatua hiyo baada ya mwaka 2015 kutokea kwa ajali dada yake ambaye alihitaji damu ya haraka zaidi na kupatiwa damu kutoka benki ya damu ila hakuweza kukaa sana na kufatiki ndipo familia ilipoamua kuhamasisha kuchangia damu kila mwaka na 2018 ikiwa ni mara ya pili.

Meneja wa Damu salama kanda ya Mashariki Dkt Avelina Mgesa amesema kuwa kwa mwaka damu lita 450,000 inahitaji ila mwaka 2016 iliweza kupatikana lita takribani 160,000 ambapo hazitoshelezi kwa mahitaji ya kila siku.