Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma
Wananchi waendelea kupatiwa msaada mbalimbali wa kisheria kupitia, kampeni ya Mama Samia Legal Aid Kampen iliyopo chini ya wizara ya wizara na sheria.
Katika kampeni hiyo watalamu wamepiga kambi kakitika maonesho ya nanenene jijini Dodoma wa sheria kambi katika maonesho ya nanenane viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma huku wananchi wakimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada huo huku wakishauri iwe taasisi ya kudumu itakayowasaidia kupata haki zao kwenye migogoro ya kisheria.
Luciana Mwanitu, kutoka munisipa ya Dodoma kata nzunguni alisema kwamba aliamuwa kufika kwenye banda hilo ili aweze kijifunza kazi zao wanazozifanya za kutoa huduma kwa wananchi.
“Nime elimishwa kuhusu huu mpango wa Mama Samia, lakini nashauri jambo moja hii ni taasis mpya na watu wengi hawafahamu kuhusu hii taasisi na kazi yake kwaiyo ni muhimu sana kuongeza elimu hii katika maeneo mbalimbali ya nchi hursa maeneo ya vijijini,” alisema.
Aidha alimpozega Rais Samia Suluhu Hassaba Kwa kutoa huduma ya elimu kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid, huduma hi ni muhimu sana kwa wananchi kwasababu wapo watu wengi wanashindwa kupata haki zao kwa kukosa msaada wa kisheria.
Mwananchi mwingine, Renatha Manda mkazi wa amesema ametembelea banda hili la sheria la Mama Samia na amekutana na maofisa wamempatia msaada wa kisheria.
“Nashukuru sana nilkuwa tatizo la kisheria lakini nimekuja hapa nimepatia msaada wa kisheria na tatizo limeisha, Pia nimepatiea ushauri na elimu nzuri kuhusu masuala ya kisheria na najipanga vizuri kwenye kuweka mirathi.”
Amesema mpango huo ni mzuri katika kuwasaidia wananchi wasio na uwezo ambao hawana uwezo wa kuweka Mawakili.
Katika Maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kukutana na wataalamu wa sheria ambao wanaweza kuwasaidia kuelewa na kutatua matatizo yao.
Mkazi wa Shinyanga mjini, Uwezo Maulid,amesema alimuwa kuja nanenane kwenye banda hilo asaidiwe apate haki ya mirathi ya mume wake.
Mume wangu alikuwa mtumishi wa umma katika manispa ya Shinyanga, nilienda mahakamani ili wanagu na mimi mwenyewe tupate haki kuhusu maali ya maremu lakini sitendewi haki.Huu ni mwaka wa nne tangu marehemu afariki lakini mpaka dakika hii sijapata hata shilingi mia alizoacha marehemu mume wangu nakatika ka nyumba tulikiwa tunaishi nimefukuzwa na baba wa marehemu na kunitihisha,”alisema.
“Nimekuja hapa ili nisaidiwe,mimi na wanagu tupate msaada wa kisheria na ninaamini nitasaidiwa.
Mwisho