Mahakama ya kijeshi imewahukumu wanajeshi 10 vifungo vya kati ya miaka saba na maisha kutokana na ghasia ambapo mwandishi wa habari aliuawa na wafanyakazi wa kutoa huduma za kibinadamu kubakwa.

Mahakama imeiamrisha serikali ya Sudan Kusini kumlipa kila muathiriwa wa ubakaji dola 4,000 kama fidia.

Uhalifu huo ulitokea wakati wa shambulizi lililofanywa katika hoteli ya Terrain kwenye mji mkuu Juba mwaka 2016.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliwalaumu walinda amani kwa kushindwa kuitikia msaada wa waathiriwa.

Wanajeshi wa Sudan Kusini wamelaumiwa kwa kuendesha uhalifu mara kadhaa tangu yazuke mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 lakini hili ndilo lilikuwa shambulizi baya zaidi dhidi ya raia wa kigeni.

Hii ndiyi mara ya kwanza wanajeshi wameshukiwa kwa kuendesha uovu Sudan Kusini, taifa janga zaidi duniani ambalo lilipata uhusu wake mwaka 2011.

Mahakama iliiamrisha serikali iilipe familia ya mwandishi wa habari John Gatluak ngombe 51 kama fidia.

Alikuwa akichukua hifadhi kwenye hoteli hiyo wakati aliuawa.

Wanajeshi wawili walipatikana na hatia ya kumuua na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Wengine watatu walipatikana na hatia ya kuwabaka wafanyakazi wa kuto misaada, wanne kwa dhuluma za kingono na mwingine kwa wizi wa kutumia nguvu.

Walihukumiwa kati ya vifungo vya miaka 7 na 14 jela.

Shambulizi hilo lilifanyika wakati wa mapigano makubwa mjini Juba kati ya vikosi vya serikali na vile vya waasi.

Zaidi ya watu 70 wakiwemo wakiwemo walinda amani wawili wa Umoja wa Mataifa waliuawa wakati wa mapigano ya siku tatu.