Takriban wanajeshi 36 wa Nigeria wameuwawa katika mashambulizi mawili wakati wa operesheni dhidi ya magenge yenye silaha huko katika jimbo la kaskazini ya kati la Niger.
Wanajeshi hao wameuawa kufuatia mashambulizi mawili wakati wa operesheni dhidi ya magenge yenye silaha katika jimbo la kaskazini ya kati la Niger.
Msemaji wa jeshi Meja Jenerali Edward Buba amesema katika mkasa wa mwanzo waliuwawa ni pamoja na maafisa watatu na askari 22, askari wengine saba walijeruhiwa katika shambulizi hilo la kuvizia.
Aidha Buba amesema katika operesheni tofauti ya kijeshi katika jimbo la Kaduna, askari walifanikiwa kuwaokoa mateka 10 waliozuiliwa katika kijiji kimoja na kuwaua watekaji nyara wao baada ya makabiliano makali.
Katika kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita magenge ya watu wenye kujihami kwa silaha nzito yamesababisha maafa makubwa katika eneo la kaskazini magharibi mwa Nigeria kwa kuwateka nyara maelfu, kuua mamia na kuvuruga usalama wa barabarani.