Wanafunzi 17 kutoka shule tano katika Jimbo la Yobe, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wamekufa kufuatia mlipuko wa homa ya uti wa mgongo, mamlaka inathibitisha.
Miongoni mwa wanafunzi hao, wapo wa shule za msingi na sekondari za bweni, kamishna wa elimu wa serikali ameeleza.
Folasade Adefisayo alisema jumla ya kesi 473 zimerekodiwa hadi sasa.
Homa ya uti wa mgongo ni maambukizi ambayo husababisha kuvimba kwa tabaka za nje za ubongo na uti wa mgongo.
Imeelezwa ugonjwa huo unaweza kuhatarisha maisha isipokuwa kutambuliwa na kutibiwa mapema