Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

Ujenzi wa Mradi wa Miji 28 Chamwino, Mkoa wa Dodoma unaendelea ambapo visima 8 vitakavyopeleka maji kwenye tanki la kuvunia maji vimekamilika.

Kazi inayoendelea kwa sasa ni ujenzi wa matanki mawili ya lita laki mbili (200,000) eneo la Msanga, tanki la kuvunia maji la lita laki tano (500,000) katika eneo la Chamwino na ujenzi wa kituo cha kusukumia maji eneo la Chamwino.

 Fundi kutoka  Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akisuka nondo wakati wa ujenzi wa tanki la kuvunia maji la lita laki tano (500,000) kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.

Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake. 

Mradi huu unatekelezwa chini ya Wizara ya Maji ambapo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ni miongoni mwa wanufaika katika kanda yake ya Chamwino.

Akizungumza jana Kaimu Meneja wa Chamwino, Gray Mbalikila amesema Mji wa Chamwino unakua kwa kasi, hivyo kupitia mradi huu hali ya maji itaimarika zaidi na kuweza kusogeza huduma maeneo ya pembezoni ambayo yanakua kwa kasi zaidi kwa sababu uzalishaji wa maji utaongezeka na miundombinu ya mabomba itaboreshwa zaidi.

“Mradi huu unahusisha kazi ya uchimbaji na uendelezaji wa visima virefu ambavyo vinapatikana katika eneo la bonde la maji la Chamwino, ujenzi wa tanki la kuvunia maji katika eneo la Chamwino lenye ujazo wa lita laki tano. Tanki hili litakusanya maji kutoka kwenye visima virefu 8,” amesema Mbalikila

Pia ujenzi wa kituo kikuu cha kusukumia maji kwenda katika tanki la Buigiri lenye ujazo wa lita milioni mbili na laki tano (2,500,000) na tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga.

Kazi nyingine ni usambazaji wa maji kwenda katika eneo la huduma yakitokea kwenye tanki la Buigiri kwa bomba kubwa kwenda katika maeneo ya Buigiri, Chinangali II, Mwegamile na Chamwino na usambazaji wa maji kutoka kwenye tanki la Msanga kwenda katika maene.

Fundi kutoka  Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akifanya vipimo wakati ujenzi wa kituo cha kusukumia maji kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.
Fundi kutoka  Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akiendelea na ujenzi wa tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.
Mafundi kutoka  Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India wakiendelea na ujenzi wa tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.