Na Magrethy Katengu, JamuhuriMedia,
Dar es Salaam
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Allience far Democratic clChange (ADC), wamepinga matokeo ya uchaguzi ndani chama hiko uliofanyika Juni 29,2024 huku wakikata rufaa wakidai kuwa tangu zoezi la hilo lianze kumekuwa na ukiukwaji wa katiba ya chama hiko.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Julai 1,2024 Jijini Dar es salaam aliyekuwa katibu mkuu wa chama hiko ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti Taifa ADC, Doyo Hassan Doyo, amesema mkutano huo mkuu wa ichaguzi ulighubikwa na madhila mengi kulikuwa na ubaguzi baina ya wajumbe na kanuni za chama zikivunjwa waziwazi.
Doyo amesema wao wamefanya uamuzi kupeleka barua yao ya rufaa Juni 30,2024 saa kumi jioni katika kamati ya rufaa ya chama ambapo kikatiba inamruhusu mgombea yeyote baada matokeo kutangazwa kama ana malalamiko kuhusu uchaguzi anaruhusiwa kuandika maelezo ndani ya masaa 24 .
“Mimi mgombea wa uenyekiti na wanachama wenzangu pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu zaidi ya 70 tunapinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Juni 29,2024 kutokana na sababu ikiwemo kukiukwa katiba chama ambapo inasema Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utaongozo na Mwenyekiti wa muda atakayechaguliwa lakini haikuwa hivyo Mkutano ule uliongozwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hamadi Rashidi Mohamed hoja yetu ya rufaa tunahoji kateuliwa na nani kuendesha mkutano ule na hakukua na tamko lolote” amesema.
Hata hivyo amebaisha kuwa Hamadi Rashidi Mohamedi aliongoza mkutano kimakosa hivyo alivunja kanuni za chama na wao hawalalamikii matokeo bali ni ukiukwaji wa kanuni zilizo kwenye katiba yao hivyo hayo mapungufu ya kikanuni wakifumbia macho itapelekea chama kisisimame hata kama wao hawatakuwepo kitavurugika.
Doyo amesema yeye wanachama wenzake wamepinga uendeshaji uchaguzi, matokeo na ukiukwaji wa katiba na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kutojiazuru na kuendelea kuhodhi madaraka na genge lake kwani kwakuwa yeye ni muasisi wa chama na ana kadi no 2 anaifahamu katiba hawezi kushuhudia kuona Hamadi Rashid Mohamed na genge lake kumvisha kanzu akiwa anaona.
” Uchaguzi huu ulishangaza kura kuongezeka kuvuka namba ya wajumbe walipo 192 kutoka nchi nzima hadi majina ya orodha ya watu yalipo kwenye daftari lakini waliingi 240 wanaofahamika ndipo tulipongea Mwenyekiti huyo akaomba tukae kimya ndipo akaamuru watu wote watake nje na kuingia wajumbe 168 lakini bado walioingia wengine majina yao hayapo kwenye orodha bali majina mapya yalisajiliwa mlangoni na kura zilipopigwa idadi ilizidi hivyo wizi ulifanyika kumuongezea mgombea mwenza ushindi hivyo hatukubali na baadhi ya wanachama wenzangu walipewa madaraka wameyakata na tumeungana kusema uchaguzi hakuheshimu katiba” amesema Doyo
Sanjari na hayo wamebaini kuwa Hamadi anataka kufanya chama hiko kuwa cha familia ambapo ikiangaliwa Mwenyekiti wa Zanzibar ni Mtoto wake, Mkurugenzi wa fedha mdogo wake wamezaliwa mama,baba mmoja Makamu mwenyekiti bara Hassan Mvungi Dereva wake ,Mkurugenzi wa Mambo ya Nje mkwewe aliyemuoa mwanae hivyo huo ni uongozi aliouteua kukigeuza chama kuwa cha familia.
Naye Shara Amrani Khamisi aliyekuwa Mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti Zanzibar amesema mwanaye Hamadi Rashid Mohamedi alikuwa na nia ya kugombea Uwenyekiti lakini baada ya kuona Hassan Doyo anagombea na hawezi kusimama naye badala yake Hamad alimpigia simu na kumwomba hiyo nafasi ya Mgombea Makamu mwenyekiti Zanzibar asigombee lakini kikatiba ni haki yake hakukata tamaa alisubiria baada ya siku mbili akaenda kuchukua fomu .
” Ninashangazwa ni Kiongozi gani anakwenda kumsitisha mtu na ana haki kikatiba kugombea? sawa na wengine ilivyofika nahitaji wadhamini nilipambana mpaka jasho nipewe watu waliko kwenye daftari ambalo siwezi kuliingilia nikapiga simu sipokelewi,nikaandika ujumbe sijibiwi baadae nikaandika ujumbe mkali ambao mpaka leo ninao kwa naibu katibu mkuu Sandip wakapigiana simu na kukubali kunipatia wadhamini” amesema Shara.
Shara amebainisha kuwa tokea mwanzo lengo la kuwanyima wadhamini lilikuwepo na walipokuja wakitokea Pemba waliletwa na ulinzi mkali wakawekwa kwenye chumba kimoja walisimama nje wakiomba kuingia ili wakasainiwe fomu baada ya kuona hakuna mafanikio ndipo miongoni mwao mmoja alijaribu kutumia nguvu alisukumwa na kuangushwa chini hivyo kwa kweli jambo hilo likifumbiwa macho ubaguzi,udhalilishaji,uonevu,ubinafsi vitu hivyo vikiachwa chama sijui kitakuwa mwelekeo gani.