Mwandishi wetu.maipac
[email protected]

Dar es salaam.Wamiliki wa vyombo vya habari nchini,wametakiwa kuwalipa malimbikizo ya madai wafanyakazi wao wanaowadai na kutoa mikabata ya ajira ili kuongeza Uhuru wa habari na kujieleza nchini.

Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa ldara ya Habari Maelezo, Bw.Thobias Makoba alitoa wito huo juzi wakati anafungua kongamano la Uhuru wa kujieleza na sheria za habari nchini,lililoandaliwa na Mtandao wa watetezi wa Haki za binaadamu nchini (THRDC).

Makoba alisema serikali inajua changamoto ambazo zinakabili vyombo vya habari ikiwepo suala la kiuchumi hata hivyo wakati serikali Inaendelea na mchakato wa kulipa madeni yake kwa vyombo vya habari vyombo hivyo vinapaswa kuwalipa wafanyakazi.

“Tunajua kuna madai Sasa tukilipa tunaomba muwalipe na wafanyakazi wetu ili wafanyakazi waweze kufanya kazi zao vizuri”alisema

Akizungumzia sheria za habari nchini,alisema serikali Inaendelea na mchakato wa maboresho ya sheria ikiwepo kuundwa kwa Bodi ya Ithibati,Baraza huru la habari na mfuko wa kusaidia wanahabari.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa chama Cha Wafanyakazi Katika Vyombo vya habari Nchini(JOWUTA) Mussa Juma aliomba serikali kusimamia sheria a katika suala la malipo ya wanahabari na mikataba.

Alisema asilimia 80 ya waandishi wa habari nchini hawana ajira na mikataba ya kazi hali ambayo inaathiri Uhuru wao wa kufanya kazi.

Juma ambaye pia Mkurugenzi wa Taasisi ya wanahabari ya MAIPAC alishauri Idara ya Habari Maelezo pia kufanya tathmini na ufatiliaji wa mara kwa mara ya Utendaji kazi wa wanahabari na Hali ya vyombo vya habari kama zilivyotasnia nyingine.

Awali Mratibu wa Kitaifa wa watetezi wa Haki za binaadamu nchini(THRDC)Onesmo Ole Ngurumwa alisema kuna mapungufu katika sheria kadhaa za habari nchini ambazo zinaminya Uhuru wa kujieleza.

Ole Ngurumwa alisema sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Clime Act 2015)Sheria ya huduma za habari (MSA 2016),Sheria ya Takwimu na sheria nyingine kadhaa ili kusaidia kukuza Uhuru wa kujieleza nchini.

Akizungumza katika mkutano huo. Balozi wa Marekani, Michael Battle alisema serikali ya Marekani itaendelea kusaidia kuendeleza Uhuru wa kujieleza nchini Tanzania.

Battle alisema kiasi cha dola 250,000 zaidi ya million 650 zimetengwa na serikali ya Marekani kusaidia masuala ya Uhuru wa kujieleza hapa nchini na uhuru wa vyombo vya habari.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) Kenneth Simbaya alisema wanashukuru serikali kuendelea kuboresha Uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Alisema tofauti na miaka nyuma sasa serikali imefungua milango ya kuendelea na majadiliano ya kuboresha sheria za habari lakini pia kuboresha mazingira ya wanahabari kufanya kazi .

Kongamano hilo lilishirikisha wanahabari na aww wadau wa habari wa ndani na nje ya nchi na lilidhaminiwa na Taasisi ya kimataifa ya ABA ya nchini Marekani.