Na Happy Lazaro, JamhuriMedia, Arusha

Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wameshauriwa kuwapeleka wafanyakazi wao katika Chuo cha ustawi wa jamii kampasi ya Kisangiro wilayani Mwanga ili wakajifunze mbinu bora za malezi ya watoto wadogo na kuwezesha kuwa na watoto walioandaliwa vizuri katika makuzi yao.

Hayo yamesemwa leo na Meneja wa Kampasi Chuo cha Ustawi wa Jamii -Kisangara Dkt Leah Mwaisango, kwenye mabanda ya maonyesho ya maandalizi ya Siku ya Wanawake inayoadhimishwa kitaifa jijini Arusha,alipokuwa akielezea hatua mbalimbali za maandalizi ya wataalamu wa malezi ya vituo vya watoto nchini.

Meneja wa Kampasi Chuo cha Ustawi wa Jamii -Kisangara Dk Leah Mwaisango akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma wanazotoa

Amesema chuo hicho kina Kampasi mbili ikiwemo ya Kijitonyama Jijini Dar es Salaamu na nyingine Kisangara.

Amesema kuwa,chuo hicho kinawaandaa wataalamu wa malezi ya watoto kuanzia ngazi ya cheti hadi Diploma ambapo wanafundishwa kwa vitendo namna ya kuhudumia watoto na kuwaandaa kwa ajili ya kujifunza .

Ameongeza kuwa ,mtaalamu anaandaliwa kumfundisha mtoto kujifunza fani mbalimbali kwa kutumia vizibo vya kuchezea ambavyo vinamchangamsha na kuanza kujifunza kuhesabu kabla ya kujiunga na mfumo rasmi wa elimu.

Amesema kuwaChuo kinatoa Kozi za mbalimbali za malezi,makuzi lishe ulinzi wa mtoto hiyo hivyo na wakati wa kuwekeza kwenye malezi na makuzi ya watoto ni sasa .

Amesisitiza kuwa, Chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya malezi kwa Vituo mbalimbali vya kulelea watoto Nchini lengo ni kuwaandaa watoto kabla ya kuanza shule

Amesema Chuo pia kipo tayari kutoa mafunzo kwa walezi wa watoto majumbani hivyo akaiomba Jamii kuanzisha vikundi ili Chuo kiweze kutoa mafunzo ya ulezi wa watoto.

“chuo kinajaribu kuangalia na kuhamasisha wazazi kuunda vikundi katika Jamii waweze kupata kozi ziweze kusaidia malezi ya watoto majumbani kwani ni wakati mazuri wa kuwekeza katika mazingira makuzi ya watoto.”amesema .

Kozi hizo zinamwezesha anayesoma maswala malezi ya awali ya mtoto ya lishe mtoto ,saikolojia ya mtoto,Ulinzi wa mtoto,maendeleo ya awali ya mtoto uchangamfu, miaka nane kushuka chini kumlea mtoto ulinzi uchangamshi .

Ameongeza kuwa,chuo kinasaidia katika malezi ya kila siku na wanajaribu kuangalia watafikiaje jamii katika ngazi ya kaya .