Mshambuliaji wa Arsenal 'the Gunners', Theo Walcot, anasema kuwa hajakosana na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Arsene Wenger, na kuongeza kwamba hajaanza mazungumzo ya mkataba mpya na klabu hiyo.
Mkataba wa Walcot unakamilika mwaka 2016 na Wenger amesema kuwa anatarajia kuwa na muda mrefu wa makubaliano na mchezaji huyo kuhusishwa kuwa atamtosa na kumsajili Marco Reus wa Borussia Dortmund.
“'Ripoti zinazosema nimekosana na kocha juu ya mkataba ni upuzi mtupu,” anasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na kuongeza: “Hatujaanza mazungumzo yoyote juu ya mkataba wangu, na lengo langu kuu ni kufanya vyema katika klabu hii.”