Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Epvate & Fortune International Consultant Ltd wameendesha mafunzo kazi ya siku mbili kwa Wakuu wa Vitengo na Wasimamizi wa Wodi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kazi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Leila Komba amesema mafunzo haya ambayo yatafanyika kwa makundi tofati yataongeza weledi na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Tuyape umuhimu mafunzo haya kwani ulivyoingia sio kama utakavyotoka, sisi kama watendaji ndio injini ya hospitali hivyo tunakutana na wafanyakazi moja kwa moja,”amesema Komba.
Naye Upendo Mwansile ambaye ni msimamizi wa wodi tatu iliyopo Jengo la Mwaisela ameushukuru uongozi wa MNH kuandaa mafunzo hayo yatakayoongeza chachu ya utendaji.