Marais 25 wa nchi za Afrika wanatarajiwa kushiriki katika mkutano wa nchi za Afrika kuhusu Nishati utakaofanyika Januari 27 na 28 mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo amebainisha hayo leo Januari 25, 2024 na wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Balozi Kombo amesema ujio wa marais hao ni rekodi aliyoifanya Rais Samia Suluhu Hassan kuwakutanisha wakuu wa nchi wengi akibainisha kuwa rekodi ya mwisho ilikuwa wakati wa Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere ambapo Wakuu wa nchi 19 walifika nchini.

Pamoja na mambo mengine, miongoni mwa malengo ya mkutano huo ni kuwafikia watu milioni 300 kupata nishato ya Umeme barani Afrika ifikapo mwaka 2030 kutokana na takwimu kueleza kwa sasa watu milioni 600 hawana nishati hiyo.