Na Cresensia Kapinga,Namtumbo.
Wakulima wa zao la mahindi mkoani Ruvuma wameiomba Serikali ione umuhimu wa kuweka bei ya zao hilo ambayo inafafana na gharama ya uzalishaji tofauti na hivi sasa kilo moja ya mahindi wakala wa hifadhi ya chakula kanda ya Songea(NFRA) inanunua kwa kiasi cha sh. 800 kwa kilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari wakulima hao walisema kuwa tangu msimu wa ununuzi wa mahindi ulipoanza bado wanaendelea kuiomba Serikali iangalie uwezekano wa kupandisha bei kutoka sh. 800 hadi 1000 kama ilivyokuwa kwa mikoa mingine hapa nchini.
Bw. Salum Mohamedi mkazi wa kijiji cha Lwinga wilayani Namtumbo amesema kuwa tatizo kubwa lililopo kwa hivi sasa ni bei ya mahindi ambayo NFRA inanunu ni ndogo ambayo hailingani na gharama za uzalishaji wa zao hilo hivyo ameiomba serikali iangalie namna ya kuongeza ili mkulima anapouza mahindi yake asiwe na machungu kwani hata bei hiyo mkulima akiuza mahindi yake kumekuwa na makato baada ya kuuza mahindi hayo.
“Ndugu waandishi bei ya mahindi ni ndogo ikilinganishwa na gharama tulizotumia kulima,kununua pembejeo pamoja na gharama za usafiri wa kusafirisha mazao kutoka shambani hadi nyumbani na kuyapeleka kwenye kituo cha ununuzi wa mahindi kilichowekwa na NFRA hakikidhi mahitaji.’’amesema Mohamed.
Amesema kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto ya makato ambapo ukipiga hesabu baada ya kuuza zaohilo unakuwa umeuza kwa kiasi cha sh.600hadi 700 kwa kilo jambo ambalo linawashusha moyo wakulima kuendelea kupeleka mzigo kwenye gharana badala yake wanapeleka kwa wafanyabiahara ambao wa mahindi wananunua mahindi bila ya kuwepo makato ya aina yeyote kwa sh. 800.
Amefafanua zaidi kuwa licha ya kuwa unapeleka mahindi kuuza NFRA bado kunaucheleweshwaji wa malipo kwani mkulima kwa kuwa amekuwa na matatizo mengi anatamani akiuza mahindi yake alipwe fedha papo hapo tofauti na ilivyo hivi sasa mkulima anapeleka mahindi alafu anaambiwa asubiri.
“Ombi langu kwa serikali kupitia waziri mwenye dhamana kurekebisha utaratibu wa makato kwaamaana kuwa kama bei ni sh. 800 basi ibaki bei hiyo hiyo ili naye aebdele na moyo wa kuleta mzigo wa mahindi kwenye ghala.” amesema.
Naye Maimuna Hussein mkazi wa kijiji cha Namabengo wilayani Namtumbo ameiomba Serikali kupitia waziri mwenye dhamana kuangalia namna ya kuweka bei ya ununuzi wa zao la mahindi iwe inalingana na mikoa mingine tofauti na hivi sasa bei ya kilo moja kwa mkoa wa Ruvuma ni sh. 800 wakati katik mikoa ya kaskazini mahindiyananunuliwa kwa kilo moja sh. 1000 jambo mbalo wakulima wameshindwa kuelewa kuwa wanaponunua bei ya mbolea ni elekezi kwa nchi nzima lakini wakati unauza mazao bei zinakuwa tofauti.
Mkuu wa kituo cha ununuzi wa mahindi cha Namabengo kutoka NFRA Bw. Lugano Moses ameshauri wakulima kwenda kuuza mahindi yao NFRA badala ya kuuza mahindi yao kwa wafanyabiashara kwani serikali inanunua kwa bei nzuri na malipo yanalipwa kwa wakati na si vinginevyo.
Kwa upande wake meneja wa wakala wa hifadhi ya chakula Taifa (NFRA) kanda ya Songea Zenobius Kahele akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake alisema kuwa NFRA ilishaanza kununua mahindi tangu msimu umeanza licha ya kuwepo changamoto ndogo ndogo ambazo zimeendela kufanyiwa kazi na kwamba hali ya ununuzi wa mahindi sio mbaya japo baadhi ya vituo kutoka Wilaya ya Nyasa na Tunduru vilishafungwa kutokana na zao hilo kutokuwepo na kwamba katika maeneo mengine zoezi la kununua mahindi linaendelea licha ya kuwepo kwa baadhi ya wanaoleta mahindi hawaangalii ubora yamekuwa na unyevu unyevu jambo ambalo limeonekana kuwa ni kero kwenye zoezi hilo la kununa mahindi.