Baadhi ya wageni hao wamediriki kuendesha shughuli za ufugaji katika Hifadhi ya Taifa Serengeti (SENAPA), na kilimo katika vijiji vya Tarafa ya Loliondo. Matrekta mengi yanayotumiwa katika kilimo eneo la Loliondo yanatolewa Kenya.
JAMHURI limepata majina zaidi ya 280 ya Wakenya wanaoishi Ngorongoro, ambao baadhi yao wamekimbia wakihofu uongozi mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli.
Pamoja na kuingia hadi SENAPA, Wakenya hao wamekuwa wakinunua mashamba na kuendesha kilimo katika Pori Tengefu la Loliondo na hivyo kuhatarisha uhifadhi katika eneo hilo.
Utambuzi wa wageni hao umekuwa mgumu kwa vile hawana tofauti ya ki-mwonekano na hata lugha na wenzao wa Tanzania. Viongozi kadhaa wa Tanzania wanatuhumiwa kuwapokea na kuwalinda.
Imebainika kuwa miongoni mwao wanajihusisha moja kwa moja kwenye uanzishaji na uendeshaji wa asasi zisizo za serikali (NGOs) ambazo zimekuwa ndiyo ‘watalawa’ wa Loliondo kwa kivuli cha utetezi wa wafugaji.
Kwa kutumia mashirika hayo, wamefanikiwa kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kupitia ufadhili; na wakati huo huo kuutumia mwanya wa utetezi wa wafugaji kuingiza maelfu ya mifugo kutoka Kenya.
Mwaka jana sehemu ya mifugo hiyo iliyokuwa ndani ya SENAPA iliondolewa baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Hashim Shaibu.
Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa wahamiaji na walowezi hao haramu wengi wao wanaishi na kuendesha shughuli katika kata za Engaresero, Orgosorok, Oloipir, Oloirien-Magaiduru, Oloosoito-Maaloni na Ololosokwan.
Kuwapo kwa Wakenya hao Loliondo kunatajwa kusababisha athari nyingi za kiusalama na kiuchumi. Athari hizo zinaonekana wazi katika eneo la Wasso ambako mamia ya wageni wamemilikishwa ardhi na kujenga nyumba za kuishi na za kibiashara.
Katika Kijiji cha Ololosokwan, Wakenya hao wapo katika vitongoji vya Osero Sopia, Eng’ong Nairouwa (Maji Moto), Kururu, Olorien, na Enting’iting.
Operesheni iliyoendeshwa hivi karibuni na vyombo vya ulinzi na usalama katika Wilaya ya Ngorongoro ilibaini Wakenya zaidi ya 60 wenye maelfu ya ng’ombe, mbuzi na kondoo ndani ya SENAPA. Wafugaji hao wa kigeni walikutwa hadi kilometa 10 ndani ya Hifadhi hiyo yenye umaarufu wa kipekee duniani.
DC Hashim, amezungumza na JAMHURI na kusema pamoja na vikwazo anavyopambana navyo, amehakikisha anapunguza tatizo la wahamiaji haramu ambalo anasema lilishaota mizizi.
“Nipo hapa kuyatambua na kuyalinda maslahi ya Tanzania na wananchi wa Tanzania. Hatuwakatai wageni, lakini wanapaswa waingie nchini na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Kazi hii ni ngumu, lakini nashukuru napata ushirikiano kutoka kwa vyombo vyote,” amesema Hashim ambaye kwa muda mfupi aliokaa Ngorongoro amenyoosha mambo mengi.
Amesema baadhi ya watu waliotambuliwa kuwa ni Wakenya wamesharejeshwa kwao kwa kufuata sheria na taratibu za kitaifa na kimataifa.
Uchunguzi wa JAMHURI umefanikiwa kuwatambua wavamizi hao. Majina yao na maeneo wanakotoka nchini Kenya ni kama ifuatavyo:
1: Moiyare Laleta
2: Ole Kairung’u (Naikara)
3: Zakaria Narikay (Embash)
4: Ole Nkai Kapiro (Kenya)
5. Ole Toroge Naikara
6: Ole Shunguru (Embash)
7: Ole Kirigany (Ngusero Sambu, Tanzania)
8: Oloosekenge Reiya (Embash)
9: Ole Engo (Losekengei)
10: Ole Rikaiyan (Esoit)
11: Ole Nkuruna (Olderkesi)
12: Olorgeso (Embash)
13: Ole Koikai (Naroosura)
14: Ole Kimojino (Naroosura)
15: Ole Naing’isa (Naroosura)
16: Ole Ngiminisi (Naroosura)
17: Ole Rakwa (Naroosura)
18: Ole Ketuta (Kipaipaya )
19: Ole Lindi (Engusero Sambu, Tanzania)
20: Ole Ndaiya (Naroosura)
21: Ole Kinayio (Naroosura)
22: Ole Leitepa (Pusumoru)
23: Ole Koiyiee (Engusero Sambu, Tanzania)
24: Kimaa (Enkoiroroi)
25: Ole Silandoi Naroosura Ole
26: Ole Reiyia (Esoit)
27: Ololoso (Lesekengei)
28: Ole Kinayio Odoo (Naroosura)
29: Orkokoyoi Oloinyo (Olalaimutia)
30: Ole Kikonya (Olderkesi)
31: Ole Kursai (Talek)
32: Ole Kikonya (Olderkesi)
33: Ole Pirikanyi (Lalaimutia)
34: Ole Letoluo (Noonjutaa)
35: Ole Mayiani (Oldekesi)
36: Ole Ngurunaa (Posimoru)
37: Ole Sakerini (Losho)
38: Ole Murunya (Oldekesi)
39: Ole Kioko (Orkiloriti)
40: Ole Kariboloo (Oldekesi)
41: Ole Shukur (Oldisare)
42: Ole Naingisa (Mosiro)
43: Ole Ketuta (Telegutu)
43: Ole Kinayio (Osupuko) Ole
44: Ole Mundere (Naikaraa)
45: Ole Karia (Noonjuta)
46: Ole Kasoe (Olorok)
47: Miponyi Kipila (Lalamutia)
48: Ole Motire (Osupuko)
49: Nyakuni (Ngo’munisho)
50: Ole Sarite (Osupuko)
51: Ole Kindet (Lalaimutia)
52: Ole Shunguru (Naroksuraa)
53: Oldapash Masharehi (Engoilaleie)
54: Maripet Purengei (Naroksuraa)
55: Ole Koshal (Naikaraa)
56: Ole Kasoe (Ematie)
Baada ya kuondolewa ndani ya SENAPA, Wakenya hao na maelfu ya mifugo yao walihifadhiwa kwa muda katika maeneo ya Kilamben, Oloirien, Mederi/Kururu, Olooseke, Kokaa, Osero Sopia na Maji Moto.
Uchunguzi umebaini kuwapo kwa juhudi za viongozi waandamizi kutoka Kenya waliofika nchini na wengine kutuma ujumbe wakihaha ili mifugo hiyo iachiwe.
Wakenya wameanzisha Soko la Mifugo la Karkamoru katika Kata ya Oloipir huku viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro wakiwa hawajaliidhinisha. Mtetezi mkuu wa mnada huo anatajwa kuwa ni Diwani wa Soitsambu, Daniel Ngoitiko.
“Ni soko lililoanzishwa kwa nguvu za Wakenya. Halmashauri hailitambui wala hakuna ushuru unaokusanywa. Wanajaa Wakenya wanaouza na kununua ng’ombe. Wanaotetea ni baadhi ya viongozi ambao nao uraia wao una shaka,” kimesema chanzo chetu.
DC Shaibu, anakiri kuwapo wimbi kubwa la wahamiaji haramu na walowezi katika wilaya hiyo, na ahadi yake ni kwamba wataondolewa.
Katika kuthibitisha hilo kwa vitendo, amesimamia kufungwa baadhi ya maeneo ya mipakani ili kukabiliana na wimbi kubwa la wahamiaji hao ambao wamekuwa na athari kubwa kwa Loliondo na SENAPA.
Baadhi ya maeneo yaliyofungwa ni ya Ololosokwan kuelekea Posmoru ambako kuna mnada mkubwa wa mifugo unaohodhiwa na Wakenya.
DC Shaibu anasema: “Operesheni imefanyika, tumepata mafanikio makubwa. Raia 17 wa Kenya tumewakamata wakiwa na mifugo 3,510. Wengine 44 walikimbia na mifugo yao. Tuliowakamata tumewafikisha mahakamani. Tumeruhusu mifugo iachiwe kwenda Kenya. Viongozi wa Kenya wakiwamo machifu na ma-DC walifika Loliondo tukazungumza.
“Tukawambia wazi kuwa ujirani mwema ni muhimu, lakini siyo wa kuleta mifugo kuvuruga huku kwetu. Bado tunao Wakenya wengi ambao tunataka wafuate taratibu za kuishi nchini. Wananchi wetu tumeanza kuwapa elimu ili wajue athari za wahamiaji haramu. Wao wanajua hao wahamiaji ni ndugu zao, lakini tunawaambia hasara za kuwakaribisha bila kufuata taratibu na sheria. Tunaomba wananchi wote wawe wazalendo ili kulilinda Taifa letu.”
Hatua ya Shaibu ni mwendelezo wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa (RC) na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, ambaye kwa nyakati tofauti alinukuliwa akiapa kuhakikisha Loliondo inatawalika.
Ndibenda anatambua nguvu za wahamiaji na walowezi na namna wanavyotumia nguvu za fedha kupitia NGOs ili kuhakikisha Loliondo na Ngorongoro zinakuwa kwenye migogoro kwa muda wote.
Mwaka jana, aliyekuwa Diwani wa Ololosokwan, Yanik Ndoinyo, alizungumza na JAMHURI na kukiri kuwa msako mkali ulifanywa na vyombo vya ulinzi na usalama na kuwanasa raia kadhaa wa Kenya. Kata ya Ololosokwan inatajwa kuwa miongoni mwa maeneo yenye Wakenya wengi.
Kamishna wa Huduma za Uhamiaji na Udhibiti wa Mipaka, Abudallah Abdullah, amesema suala la kuwashughulikia wahamiaji haramu na walowezi katika Wilaya ya Ngorongoro limeanza na ni la kudumu.
Wamiliki ardhi kubwa
Ingawa sheria za ardhi za Tanzania zinazuia raia wa kigeni kumilikishwa ardhi, walowezi na wahamiaji haramu wanamiliki aradhi kubwa katika vijiji vya Soitsambu na Ololosokwan.
“Hapa wana ardhi kubwa kwa sababu walikotoka wanajua thamani ya ardhi. Wamefanya watu wetu wakose malisho na kwa sababu hiyo kuna migogoro ya mara kwa mara.
“Tumekuwa na vikao vya kulaani vitendo vyao vya kutaka kukigawa kijiji na wakati vikao hivyo vimesimamiwa na wazee wa mila. Umiliki wa ardhi wameupata kutokana na wao kushika nafasi katika uongozi wa kata na vijiji wao wenyewe au kwa kuwaweka wenzao wenye asili ya Kenya. Utaona hata Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana waliingia, lakini wakawekewa pingamizi. Mbaya zaidi wanaingia CCM ambako wanajua hawataguswa,” anasema mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la ole Sipai.
Uchunguzi wa JAMHURI unaonyesha kuwa wakati wa uchaguzi watuhumiwa kwa kiasi kikubwa waliingiza Wakenya wenye mifugo katika ardhi ya kijiji na kuingiza magari kutoka Kenya kwa ajili ya kuwasaidia wao na watu wao katika kampeni.
Moja ya magari aliyokuwa anatumia mmoja wa watuhumiwa ni Toyota Land Cruiser lenye usajili wa Kenya wa namba KAM 591 J.
Mtandao wao unatajwa kuwa wenye nguvu kwani hata Jeshi la Polisi, licha ya kuwa na taarifa za uhakika juu ya matukio hayo, halichukui hatua. Lawama zinaelekezwa kwa polisi wa Kituo cha Ololosokwan.
ORODHA YA WAHAMIAJI HARAMU WAKENYA WANAOISHI LOLIONDO NA KUIVURUGA SENAPA
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI katika vijiji kadhaa katika Tarafa ya Loliondo umebaini majina 224 ya Wakenya ambao, ama ni wahamiaji haramu, au walowezi. Wakenya hao wanaishi na kuendesha shughuli zao huku wakipata haki zote kama Watanzania halali. Majina ya Wakenya hao ni:
1: Peter Kiromo
2: Elizabeth Nairushiye
3: Kennedy Manyeki
4: Katikasha Kamanga
5: Risa Kamanga
6: Huho Daniel
7: Jackson Manyeki
8: Glady Kurgat
9: Elizabeth Ongetont
10: James Koromo
11: John Nzuna
12: Anna Ramasigonde
13: Omaria Lengaaki
14: Nangaya Lengaaki
15: Ndito Lengaaki
16: Kalee Saitabau
17: Najara Koleli
18: Joshua Saitabau
19: Timan Rika Yion
20: Ngopeesho Olekorkai
21: Ngisu Olenanyokie
22: Joel Siyianga
23: Sikemboi Sisi
24: Noosokono Koleli
25: Lasaru Saitabau
26: Noorkorea Sisi
27: Olemeen Ngoikor
28: Joel Lengaaki
29: Elija ole Matian
30: Joel Siyanka
31: Parkipoi Murera
32: Iman Olemetian
33: Nangida Olemen
34: Joshua Mwarabu
35: Oloibor Ngapai
36: Andrew Nkanuma
37: Sintako Nkanuma
38: Ngaina Saitabau
39: Nosilat Naingisa
40: Susana Massago (mama)
41: Binifas Massago
42: Oloongoshoka Ndaiya
43: Lengoko Saitabau
44: Modolu Yengo
45: Sirere Mpoe
46: Oleengot Engo
47: Oletimoi Stephen
48: Joshua Marabui
49: David Sais
50: Lekakiuy Sananka
51: James Massago
52: Bebi Massago
53: John Ngile
54: Ole Kileu
55: Ole Sasii
56: Joel Karori
57: Chuma Shambarao
58: Olooseenge Rea
59: Sakaria Narikai
60: Orandaya Kitipa
61: Alex David
62: Dopoi Kitipa
63: Kosia David
64: Porosooi Ndaiya
65: Boma ya Oleshung
66: Boma ya ole Serei-Kututuo
67: Boma ya Olekitipa
68: Nganuma Lemorara
69: Nganeni Lemorara
70: Ng’onene Nkanuma
71: Anna Gathu
72: Ruth Kabulunze Musomba
73: David Marko Sessat
74: Naomi Marko Sessat
75: Josephine Kuria
76: Joseph Kabulunze Musomba
77: Elizabeth Musumba
78: Marco Muhinge
79: Christine Musomba
80: Ndolee Temwee
81: Jane Koromo
82: Philipo Justus Marco
83: Pareyo Kitipa
84: Olengutie Saing’eu
85: Lekinyit Reyia
86: Esophie Parmat na ndugu zake
87: Kararit Ndaiya
88: Peter Kashal
89: Olemundere
90: Kisarunga Leitura
91: Luthia Ngelenche
92: Christine Francis William
93: Christopher Marco Sessat
94: Denis Okirigiti
95: Aizack Tura
96: Magreth Kiromo
97: Peter Robert Kiromo
98: Steven Kabulunje (dereva Hifadhini)
99: Peter Mtune Kaput
100: John ole Keroto
101: Siminde Lonyori
102: Anna Ngelenche
103: Zakayo Sesat
104: Pius Mtune Kaput
105: Emmanuel Samwel
106: Joseph Sessat
107: Estomih Manyeki
108: Joachim Manyeki
109: Felomona Mtune Kaput
110: Godfrey Kiromo
111: Godwin Mtune Kaput (Mwalimu Halmashauri)
112: Lazaro Sessat
113: Beatrice Kimoro
114: Evaline Bilechi
115: Saimon Sessat
116: Emmanuel Sassat
117: Lucy Chambii
118: George Mtune Kaput
119: Yasinta Dunya
120: Anna Cheburge
121: Joyce Marko
122: Elizabeth Robert
123: Mamiam Koira
124: Lilian John
125: Josephine Koillah
126: Sananga Cooss
127: William Sangupa
128: Coos
129: Olekoreko
130: Amos Olekoreko
131: Joseph Olekoreko
132: Joseph Sessat
133: Mery Kuyato
134: Joseph Kipkia
135: Gudito Nyange
136: Marco William Mabwa
137: Yeremia Olekoreko
138: Napirura Olengopiri
139: Mapena Olengopiri
140: Manina Olenanyika
141: Kiparian Manina
142: Emmanuel Mtune Kaput
143: Nayeilo Angangi
144: Ndina Manina
145: Moris Manina
146: Soinkei Olekumbe
147: Naaramataki Olekumbe
148: Saaloi Leshashi
149: Langoi Leshashi
150: Sabina James Kiromo
151: Rozi Kiromo
152: Lourence Kiromo
153: Emmanuel Kiromo
154: Ateiti Sumare
155: Orkedienye Kapiro
156: Saruni Ngurumwa
157: Sanare Koshara
158: Kisoku Karbolu
159: Memus Sadira
160: Nanjiko Shukur
161: Kipuri Karbolo
162: Nginandei Melejeki
163: Makoi Melejeki
164: Kanaya Karbolo
165: Napatao Meyane
166: Maripet Purengei
167: Oloishuro Kariro
168: Oleshololoi
169: Kingorosh Manatiny
170: Frank Mtune Kaput
171: Kanai Mbatiany
172: Kashing Pikoyan
173: Naingei Koikay
174: Simore Letuluko
175: Nareyo Olekandika
176: Oleniboo
177: Michael Kitipa
178: Kayo Kitipa
179: Korema Mako
180: Shukuru
181: Olonyikid Sironike
182: Olokose Kapiro
183: Karungu
184: Moriko Ngurumwa
185: Shinga Mboe
186: Olorupa Pere
187: Sangau Mbatiany
188: Kararinyayia
189: Olesironik
190: Molinge Oloso
191: Orkelese Ndaiya
192: Ntumaini Nkanuma
193: Nteetu Nkanuma
194: Kosiando Tuke
195: Sopiya Kosiando
196: Daudi Mtune Kaput
197: Juliana Mtune Kaput
198: Francis Mabwa
199: Yohana Sessat
200: Saitoti Kosiando
201: Tina Leshana
202: Shirimu Kuya
203: Ndooriti Koleli
204: Ngicha Oleneko
205: Musu Ngicha
206: Lonyokie Ngicha
207: Tiene Ngicha
208: Titio Ngicha
209: John Kamanga
210: Mbizi Ololeng’a
211: Olengaiki Olepombo
212: Joseph Siere
213: Melejeki Olemunya
214: Saitoti Ngekee
215: Lesidai Melejeki
216: Koika Melejeki
217: Mbaayi Kosiando
218: Ndima Kosiando
219: Koleli Lesite
220: John Koleli
221: Kijooli Melejeki
222: Esophip Parmwat
223: Marco Parmwat
224: Kunday Parmwat