Na Mary Margwe, Dar es Salaam

Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Jacob Siay amewataka wanachama na wananchi wote Jijini hapa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura ili kujipa uhalali na haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao ifikapo uchaguzi Mkuu Mwaka huu.

Hayo amebainisha na Kaimu Katibu huyo wa CCM Mkoa wakati alipokua akitoa elimu kwa wakazi wa Kata ya Magomeni Wilaya ya Kinondoni ambapo alisema zoezi hilo la kuboresha daftari la mpiga kura katika Mkoa huo limeanza Machi 17 na linatarajiwa kukamilika mnamo Machi 23, 2025.

Siay amesema ili Wanachama na wananchi waweze kupata haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi waowataka wakati wa uchaguzi Mkuu, wanapaswa kuhakikisha wanawanajitokeza kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura ili kupata uhalali wa kupiga kura na si vinginevyo.

Aidha Siay amesema kukamilika wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura Kwa Wanachama na wananchi wa Jiji la Dar es Salaam litasaidia kupata haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka ndani ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.

Aidha Kaimu Katibu wa CCM Mkoa huo amefafanua kuwa kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2022 Mkoa huo una jumla ya watu wapatao Mil. 5,383,728, ambao ndio Mkoa wenye makadirio ya wapiga kura wengi zaidi kuliko Mikoa yote hapa nchini.

” Mkoa wetu wa Dar Es Salaam una jumla ya watu wapatao Mil. 5,383,728 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, Mkoa wetu ndio wenye makadirio ya wapiga kura wengi zaidi kuliko Mikoa yote hapa Nchini ” amesema Jacob Siay.

” Sisi kama Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Mkoa wa Dar es salaam tumefanya hamasa ya kutosha katika wilaya zetu zote ili kuhakikisha viongozi, wanachama na wananchi wanajitokeza kwa wingi katika kuboresha taarifa zao na kuandikishwa kwa wale vijana waliofikisha umri wa kupiga kura mwaka huu” ameongeza bKaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam

Kufuatia kazi kubwa ya uhamasishaji walioifanya na kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, zimewafanya watu kuendelea kukiamini na kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi ( CCM ) ndani ya Mkoa huo.

Hata hivyo Siay amesema ni matumaini yao kuwa kama ambavyo watu wameweza kujitokeza Kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura , ndivyo hivyo hivyo watakavyojitokeza baadaye kwenye zoezi la kupiga kura.

” Ni matumaini yetu kuwa kama ambavyo watu wanaendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu, ndivyo ivyo hivyo watakavyojitokeza baadae kwenye zoezi la Uchaguzi Mkuu Mwaka huu ” amefafanua Siay.

Kaimu Katibu CCM Mkoa wa Dar es Salaam Jacob Siay