Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia,Dodoma.
Waliokuwa wajumbe 18 wa Kamati tendaji ya Chama cha Walimu nchini CWT ambao wameenguliwa kwenye nafasi hizo wamemuomba Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro ambao unaendelea ndani ya chama hicho.
Kuenguliwa kwa wajumbe hao kunatokana na wao kuazimia kumsimamisha Katibu Mkuu wa CWT Taifa,Japhet Maganga kutojihusisha na shughuli zote za Chama mnamo Juni 6, 2023.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Juni 19,2023 Jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa CWT Taifa Joseph Msalaba kuhusu ufafanuzi juu ya ukiukwaji wa Katiba ya CWT toleo la 6 la Mwaka 2014 na kanuni zake uliofanywa na Rais wa Chama hicho juni 6,2023 kuwa ni batili.
Msalaba amesema kuwa kikao cha Baraza kuu la Chama hicho cha kuwaengua nafasi hizo lilikuwa ni batili na kudai kuwa lengo la Viongozi hao sio jema kutokana na kutumia madaraka yao vibaya pale tu wajumbe wanapohoji masuala ya uendeshaji wa Chama.
Licha ya hayo amesema katika mgogoro uliopo wamekuwa wakilalamikia masuala ya ajira kupandisha vyeo na kushusha vyeo bila kufuata taratibu za utumishi nakuvunja Katiba ya CWT ibara ya tatu kifungu cha pili (a)kinavyotaka kazi ya Kamati tendaji hiyo kuendesha na kusimamia shughuli za chama.
Hata hivyo ameyataja malalamiko mengine ni pamoja na kufanya hamisho zisizo na tija na zisizo zingatia bajeti,hali ya kimaeneo na bnila kushauriana na yeyote.
“Tuna malalamiko mengine Chama kina mahusiano yasiyoridhisha na Serikali,Kitaifa pamoja namatumizi mabaya ya madaraka mfano kitendo alichofanya Katibu Mkuu kutufungia geti Juni6 Mwaka huu2023 ni za kibaguzi,”Amesema.
Amesema licha ya jitahada kadhaa ambazo wamezifanya za kutatua migogoro hiyo hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya juu wa CWT aliyejigusa kutaka kuonyesha ushirikiano kutafuta suluhu na badala yake wamekimbilia kuitisha Baraza batili ambalo halikufuata hatua stahiki ili kujificha kwenye kichaka.
“Imani yetu sisi ni sauti ya wasio na sauti ndani ya CWT tunaona lengo la bviongozi hao si jema maana kila jambon wanalohojiwa hujkinmbilia kuwavua madaraka wanao hoji na kuwavua uanachama.,”amesema
Mbali na hayo Naibu Katibu Mkuu huyo ameyataja ameneo mbalimbali ambayo yanmekiukwa na katibu Mkuun wa CWT kwenye Katiba,kanuni na miongozo mbalimbali ikiwemo, kuvunja kanuni za cwt toleo la nne la mwaka 2015 kifungu chab 32 juu ya utatuzi wa migogoro na nidhamu kwa viongozi kwakukimbilia kikao na kuluiita Baraza batuli na kukitia hasara Chama.
Pamoja na hayo amesema eneo linguine ni kuvunja katiba ya CWT ibara ya tatu kifungu cha 22.3(f)kwakuandaa ajenda ya Baraza la Taifa badala ya Kamati ya Utendaji Taifa jambo linalo tafsiriwa kutumia madaraka vibaya.
“Katibu huyu amekiuka maelekeo toka Ofisi ya Waziri Mkuu yenye kumbukumbu namaba DA27/380/12/94 yenye kichwa cha habari utekelezaji wa majukumu yaChama kwakuzingatia Katiba na kanuni za CWT.
Amesema barua hiyo ilibadilishwa na Baraza hilo Juni18 2023kwakuwa ilipitishwa bila kupangwa na Kamati tendaji jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
Pia ametoa pole kwa wanachama wa CWT,viongozi mbalimbali wa chama na Serikali ambao wameumizwa na mgogoro unaoendelea ndani ya Chama hicho.
Kwa upande wake Mwakilishi wa walimu Mkoa wa Njombe Mwalimu Tobias Sanga ameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro huo kwa kuunda Tume ya kuchunguza mgogoro ili walimu wafanye kazi kutokana na walimu kutumia muda mwingi kujadili mgogoro huo.
“Walimu wamekuwa hawana kazi yakufanya zaidi ya kulumbana na kutaka suluhu,tunaomba serikali ifanye maamuzi ili shughuli nyingine ziendeleem”.Amesema.
Naye aliyekuwa Kaimu Mweka Hazina wa CWT Magesa Protus amesema kuwa migogoro ya Chama hicho inatokana na kutozingatia ushauri wa kifedha ambao alikuwa akiutoa kwa nafasi yake .
Amesema pale alipokuwa akihoji matumizi ya fedha alionekana kama mtovu wa nidhamu na hivyo kuchukuliwa kama msaliti na kupelekea kutolewa kwenye nafasi yake.
“fedha nyingi zilikuwa zikipotea bila mpangilio sikuweza kukaa kimya kuona fedha za Walimu masikini zikipotea bila matumizi sahihi,kikao kimoja kilitumia gharama ya Milioni 400 hadi Milioni800 ukihoji Katibu Mkuu anasema hakuna wakumfanya lolote,hatuko tayari kuona tunafanya kazi ya laana,”amesema.