Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia
Jumuiya na Taasisi za Kislaam Tanzania Islamic Education Panel, imetaka Serikali kuepuka hujuma na uvunjifu wa katiba unaofanywa na baadhi ya watendaji wake wachache katika suala la mitaala.
Akizungumza na wanahabari Amir Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania alhajj Musa Kundecha, amesma Serikali ina nia nzuri kabisa lakini watendaji wake wachache wanataka kutumia vibaya nafasi zao kwa kufanya hujuma kwenye suala zima la mitaala ya masomo ya dini ya kislaam.
Kundecha amedai pamoja na makubaliano na vikao muktasari walivyofanya na kukubalina lakini,muktasali uliopo sasa hivi kwenye tovuti ya wizara hauendani na makubaliano hayo hivyo wanapendekeza uondolewe haraka ili kulinda utulivu.
Amesema awali walishakubaliana kwamba suala la umiliki wa mtaala ya somo la elimu ya dini,litabaki kwa wenye dini wenyewe kama ilivyo kuwa hapo zamani huku Serikali itashirikiana na wenye dini katika kuboresha mambo ya kitaalamu.
Amesema lengo kuu la kuitisha mkutano ni kutoa mrejesho wa nini kilichotokea katika mchakato na mabadiliko ya sera ya elimu na mtaala nchini hasa katika eneo la somo la elimu ya dini ya kiislam na nini kinachoendelea ili kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki vyema kulinda umoja mshikamano baina ya Waislam Serikali na jamii kwa ujumla.
Kundecha amedai katika yao walieleza jinsi gani Serikali imesitisha mchakato wa kuandaa mihutasali ya EDK na vitabu vya kiada na kwamba waislam wawe na amani liko kwenye mikono salama.
Taasisi za kiislam zilifanya juhudi za kuweka sawa jambo hili hasa kwenye mkutano wa Agosti 29/2023 ambao ulihudhuliwa na Mufiti Shekh Mkuu wa Tanzania, Mufti wa Zanzibar, Waziri wa Elimu, Naibu Katibu Mkuu wa Elimu, Kamishina wa Elimu,Mkurugenzi wa TET, maofisa na viongozi mbalimbali wakiwemo watendaji kutoka pande zote mbili.
“Katika mkutano ule maoni ya wengi yaliunga mkono kuwa suala la umiliki wa mitaala ya dini, lazima liwe chini ya wanadini wenyewe ili kila wenye dini washughulikie mafundisho ya dini zao.
Ambapo baada ya kikao hicho IEP imeendelea na mchakato wa uandaaji wa muktasari wa elimu ya dini ya kiislam wa sekondari na umekamilika tayari umewasilishwa TET kwa ajili ya hatua zinazoendela”amesema Alhajj Kundecha.
Amesema kazi ya kuandaa kitabu cha cha kwanza inaendelea,ambapo kitakuwa tayari na kutumika ifikapo Januari 2024.
Amesema wakati na michakato yote inaendelea kuna mambo yanatatiza bado, mfano wa mambo hayo ni kuwepo kiungo cha mitaala muktasali na moduli ipo mihutasari ya masomo 15 yanayofundishwa kwa sasa masomo ya dini mihtasali yake haikuwekwa kwa kuwa TET haina haki miliki ya mitaala wa dini.
“Lakini cha ajabu katika kiunga cha machapisho rasimu ya mitaala mipya na miktasali ya elimu ya sekondari ipo, mihutasari ya masomo 27 ikiwemo somo la elimu ya dini ya kislaam ambayo inaeleza hadi miliki yote ni ya serikali hadi kudurufu ni kosa kisheria bila kupata idhini ya maandishi’’ amesema Alhajj Kundecha.
Amedai kinachowatia wasiwasi zaidi ni kwamba katika kikao cha Agosti 12,2023 waziri mwenye zamana,aliomba radhi na kukiri suala hili la umiliki wa mitalaa litabaki kwa waislamu wenyewe.
“Tunachojua ni msukumo upi wa upendo na wema unaopelekea kuvunja katiba ya nchi,kukiuka tulichokubalina kwenye vikao kwa nini tusiamini kama nia ovu ya kupotosha mafundisho ya dini yetu kwa sababu katika kikao na waziri miongoni mwa maudhui ni ya kikao ni suala la umiliki wa mitaala ya somo la elimu ya dini,likapitishwa litabaki kwa wenye dini kama ilivyokuwa hapo zamani kwa sababu suala la dini na Imani haviwezi kutenganishwa kwani imani ndiyo msingi wa mafundisho ya dini’’amesisitiza.