Kutokana na hasara kubwa kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine, Urusi imeimarisha idadi ya vikosi vyake kutumia wanajeshi kiasi 10,000 wa Korea Kaskazini.

Urusi inawasajili wanaume kutoka Yemen waende kupigana vita nchini Ukraine kupitia msaada wa waasik wa Houthi nchini Yemen. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Financial Times.

Gazeti hilo liliripoti jana Jumapili likiwanukuu watu wanaohusika, kwamba jeshi la Urusi lilikuwa limefanikiwa kuwageuza mamia ya wanaume wa Yemen kuwa wanajeshi kutumia operesheni ya siri ya kuwasafirisha binadamu.

Ripoti hiyo imesema baadhi ya wanaume hao waliahidiwa ajira ya mshahara mnono na uwezekano wa kupewa uraia wa Urusi. Lakini walipowasilia nchini Urusi, walishawishiwa waingie vitani wapigane upande wa jeshi la Urusi na mara moja wakapelekwa katika uwanja wa mapambano nchini Ukraine.

Mkataba wa usajili uliopatikana na gazeti hilo umeashiria kwamba usajili umekuwa ikifanyika tangu mapema mwezi wa Julai.