Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar e Salaam

WAHARIRI wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wameshangazwa na kuvutiwa na faida lukuki ambazo jamii na wananchi wa mikoa minane ambao wamepitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Uganda hadi mkoani Tanga.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya semina ya nusu siku iliyoandaliwa na EACOP mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuwaeleza maendeleo ya mradi ulipofikia mpaka sasa pamoja na kuwajengea uwezo wa kuufahamu vizuri mradi na faida zake kwa Tanzania kama nchi na watu wake.

Mradi wa EACOP unaotekelezwa katika eneo lenye urefu wa kilomita 1,443 kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga nchini Tanzania unapita katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga. Kati ya kilomita hizo 296 zipo ndani ya Uganda na 1,147 zipo Tanzania.

Wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakifuatilia kwa makini wasilisho kwenye semina ya kuwajengea uwezo wa kuufahamu vizuri mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Uganda hadi mkoani Tanga nchini Tanzania, iliyofanyika mwishoni wa wiki jijini Dar es Salaam.

Wakizungumzia mradi huo baada ya kuelezwa hatua ambayo wamefikia, Mhariri wa Jarida la Farmer, Nevile Meena, na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), amesema semina imewafungua macho na kuwajengea uelewa wa pamoja wa mradi na kuweza kutoa taarifa sahihi kwa umma kuhusu hatua zote za maendeleo ya mradi.

“Kazi kubwa sana imeshafanyika katika suala zima la maandalizi na wananchi wameshirikishwa ipasavyo katika eneo zima la mradi. Nikiri nimeweza kujionea mwenyewe na kiukweli nichukue nafasi hii kuwapongeza EACOP kwa kazi nzuri sana,” amesema Meena.

Amewaasa wahariri kuwa weledi na makini zaidi wanapozihariri taarifa zinazohusiana na mradi kwani faida zinazotokana na mradi huo ni nyingi kwa jamii zilizopitiwa na mradi sambamba shuhuda zinazoendelea kutolewa na wananchi.

Mkuu wa Mawasiliano wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) upande wa Tanzania, Bi Catherine Mbatia (kulia) akizungumza na Wahariri,wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini (hawapo pichani) wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wa kuufahamu vizuri mradi na faida zake kwa Tanzania na watu wake. iliyofanyikab mwishoni wa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Bw. Abbas Abraham Afisa Mawasiliano EACOP.

Mgaya Kingoba, Mhahari wa Gazeti la Serikali la Habari Leo, amesema semina imesaidia kuwajengea uwezo wa kuufahamu vizuri kwani kuna mengi ikiwemo fidia mbalimbali zilizokwisha tolewa kwa wananchi mbalimbali ambao wamepitiwa na mradi.

“Kwa hatua ya awali tumeona fidia zimeshatolewa na tumeona tayari nyumba zaidi ya 400 zimeshajengwa. Mimi kama shuhuda na weza kusema mimi binamu yangu amelipwa fidia ya shamba lake pamoja mali zote zilimo wilayani Handeni katika Mkoa wa Tanga,” amesema Kingoba.

Amesema mradi wa EACOP una maslahi mapana kwa nchi hizi mbili za Uganda na Tanzania kiuchumi na kijamii kwani mradi utasaidia kuchochea mzunguko wa pesa kutokana na ajira za moja kwa moja au vinginevyo na kule maendeleo ya haraka kwa mikoa nane inayopitiwa na mradi huo.

Khamis Mkotya, Mhariri kutoka Kituo cha Runinga cha Channel Ten mbali ya kupongeza mafunzo ya EACOP amesema yeye ni mnufaika wa moja kwa moja wa mradi huo kwani umepita katika Wilaya yake ya Chemba mkoani Dodoma na kuwanufaisha wananchi wengi wakiwemo ndugu zake.

Afisa Mawasiliano wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) upande wa Tanzania, Bw. Abbas Abraham akizungumza na Wahariri,wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini (hawapo pichani) wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wa kuufahamu vizuri mradi na faida zake kwa Tanzania na watu wake. iliyofanyika mwishoni wa wiki jijini Dar es Salaam.

“Huwa nasikitika sana ninapoona habari za upotoshaji wa mradi wa EACOP kwani ninafahamu pia nina ushuhuda nyingi kwa jamii na watu wengi walivyonufaika na mradi. Wapo waliojengewa nyumba bora na kupewa fidia ya fedha,” alisema Mkotya na kuongeza kuwa faida ya mradi nyingi kwa jamii na mwananchi mmoja mmoja na kwa serikali pia.

Amesema wahariri wasipoelewa vizuri taarifa inakuwa vigumu kufanya mawasiliano na jamii kupitia vyombo vya habari na hivyo semina hii imesaidia kuwajengea uelewa mkubwa kuhusu mradi na kuwa katika nafasi nzuri ya kuuandikia.

Hafidh Kido, Mhariri wa Gazeti la Taifa Tanzania amesema Mradi wa EACOP umekuwa na manufaa makubwa katika maeneo ya mikoa yote nane ambako mradi umepita kwani jamii husika zimeonyesha shuhuda za manufaa ya kupitiwa na mradi.

“Mafunzo haya ni muhimu sana kwani yametuvumbua macho na kutujengea uwezo wa kuufahamu mradi vizuri na maendeleo mradi ulipofikia mpaka,” amesema Kido na Kuzipongeza serikali za Uganda na Tanzania.

Akifunga semina hiyo kwa Wahariri, Mkuu wa Mawasiliano wa EACOP upande wa Tanzania, Catherine Mbatia amewashukuru wahariri kwa kujitokeza kwa wingi kwenye semina kwani itasaidia kuwa uelewa wa pamoja sambamba na kufahamu hatua mbalimbali za maendeleo ya mradi,

“Sisi kama EACOP tutafanya kazi kwa karibu sana wahariri na waandishi wote wa habari kama wadau muhimu wa mradi huu kwani mkiuelewa nyinyi (Wahariri) jamii na umma mzima wa watanzania watauelewa,” amesema Mbatia.

L