Imeelezwa kuwa, wagonjwa 6,000 wenye ugonjwa wa Hemophilia hawajatambulika, huku kati yao wagonjwa 294 pekee ndio walioanza matibabu nchini Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati wa semina kwa waandishi wa habari na wataalamu wa afya, MRATIBU Wa Kuongeza Kasi ya Upatikanaji Huduma kwa wagonjwa wa damu-Tanzania, Dkt. Stella Rwezaura amesema wanataka kuanzisha kanzi data ili kuwatambua na wakiwa jambo litakalo irahisishia serikali kupeleka huduma kulingana na idadi ya wagonjwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mkurugenzi wa Tafiti Dkt. Jessie Mbwambo amesema Novemba 2020 Muhimbili ilizindua mradi wa kuongeza kasi ya Upatikanaji huduma kwa wagonjwa wa damu, ili kuunga mkono serikali kwa upatikanaji wa huduma za Hemophilia na Selimudu katika hospitali za Rufaa.
Hata hivyo baadhi ya wazazi wa wagonjwa wa Hemophilia pamoja na wagonjwa wa hemofilia wameomba wadau wa maendeleo kuendelea kuunga mkono serikali katika kutoa dawa na vifaa tiba ambavyo vinahitaji kwa wingi huku wakilalamikia kutengwa na kunyanyapaliwa kwa baadhi ya watu wenye matatizo ya hayo katika jamii.
Hemophilia ni ugonjwa ambao, mgonjwa anatoka damu bila kuganda kutokana na ukosefu za chambe za damu ambazo husaidia damu kuganda, pindi mgonjwa anapopata jeraha.
Tatizo la Hemophilia ambalo linapelekea mtu kuvuja damu bila kusimama linatajwa kuwa moja ya changanoto hasa kutokana na wagonjwa wengi kushindwa kuripoti katika vituo vya afya ama kutokana na umbali wa upatikanaji huduma au kukosa uelewa hali inayo weza kuhatarisha maisha yao kwa sababu ya wengi wao kupoteza damu nyingi kwenye majeruhi ama kwa wanawake wakati wakiwa katika siku zao.