Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

TAKRIBANI watu  30  kati ya 200 wenye tatizo la nyonga na goti watafanyiwa upasuaji  kwenye kambi ya madaktari bingwa kwa siku nne katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).

Tangu kuanza kutolewa kwa huduma hizo katika taasisi hiyo jumla wagonjwa 5,000 wamefanyiwa upasuji wa kubadilisha nyonga na magoti na upasuaji wa magoti pekee ni wagonjwa wengi 8,000.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk Lemeri Mchome katika kambi ya upasuaji waliyoshiriki Arusha walifanya upasuaji kwa wagonjwa 104 lakini zaidi ya 50  wagonjwa wanaosubiri upasuaji wa kurudia.

“Leo tunaadhimisha miaka 20 ya upasuaji wa nyonga na magoti na katika maadhimisho haya tunafanya kambi maalum ambapo tunashirikiana na madaktari bingwa kutoka Oxford Uingereza na Austria tunajikita zaidi kwenye upasuaji wakurudi.

Amesema tangu walipoanza upasuaji miaka 20 wameshaanza kuona wagonjwa wengi ambao wanahitaji upasuaji wa kurudia,wagonjwa wenye matatizo kwenye mishipa kama uvimbe na pia wanaohitaji upasuaji maalumu.

“Hawa wa upasuaji maalum kwa miaka yote wamekuwa wakienda nje ya nchi lakini sasa MOI itaweza kufanya pasuaji hizi hapa nchini.

Ameongeza “Nitoe wito kwa wananchi ambao wanamatatizo kwamba sasa tunafungua huduma MOI tunawakaribisha waweze kupata huduma ndani ya nchi katika muda unaotakiwa bila kucheleweshwa .

Kwa upande wake daktari bingwa bobezi wa upasuaji wa mifupa na uti wa mgongo, Dk Antony Assey amesema wagonjwa nane watakaofanyiwa upasuaji ni  wa marudio na pia wagonjwa 12 wanaofanyiwa kwa mara ya kwanza.

“Takwimu zinaonesha watu wanapofika zaidi ya miaka 50 matatizo ya magoti yanaanza  umri wa 60 hadi 65 asilimia 50 watakuwa na aina fulani ya magoti na nyonga na umri unavyokwenda haja ya kufanyiwa upasuaji inajitokeza.

DK Assey ambaye pia ni mkurugenzi wa huduma za upasuaji wa mifupa MOI amesema mgonjwa akifanyiwa upasuaji baada ya miaka 15 upasuaji unarudiwa kwaajili ya kubadilisha kifaa kwasababu kinachakaa.

Daktrai Bingwa Bobezi wa Nyonga na Magoti, Dk Grey William kutoka Marekani amesema wamekuwa wakifanya kazi na nchi mbalimbali za Afrika kwa kuleta vipandikizi hasa nchini zenye kipato cha chini.

“Watu wengi huku wanateseka na matatizo hayo na wengi wanakosa vipandikizi ambazo ni za bei ghali ambazo dola 2,000.

Ameongeza: “taasisi yetu inafanya kazi na watu mbalimbali kusaidia kupata vipandikizaji ambazo tunazitumia kwa wagonjwa wetu na mafunzo hakuna faida zaidi ya moyo wa kuwasaidia wangonjwa na tunapenda hivyo,”

Please follow and like us:
Pin Share