Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Leo Juni 24, 2024 wafanyabiashara wa soko la Kariakoo wamegoma kufungua maduka wakishinikiza Serikali kutekeleza makubaliano yao waliyokubaliana mwaka jana 2023 katika kikao chao na waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Biashara pekee zinazoendelea kufanywa ni za Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama ‘Machinga’ na baadhi ya maduka machache.

Baadhi ya wafanyabiashara wamesema sababu kubwa iliyopelekea wao kufanya mgomo huo katika Soko la Kariakoo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kurudisha Kikosi Kazi (enforcement) kubwa zaidi kuliko ya awali iliyozuiliwa na Waziri Mkuu katika mkutano wa mwisho baina ya serikali na wafanyabiashara uliofanyika Mei, 2023 katika viwanja vya mnazi mmoja.

Please follow and like us:
Pin Share