Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia,
Dar es Salaam

ZAO la korosho laendelea kutafutiwa ufumbuzi wa changamoto linaloikabili katika mnyororo mzima wa thamani wa kilimo, mauzo na masoko ili kusaidia kilimo cha zao hilo kinakuwa na tija kwa wakulima kuanzia wadogo,wakati na wakubwa.

Ameyasema hayo Machi 24,2025 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE) Profesa Tandi Luwoga wakati akifungua mafunzo ya wadau wa korosho yaliyohudhuriwa na washiriki kutoka Nchi za Umoja wa Ulaya na Nchi 9 za Afrika huku Nchi 6 zikiwa ni wanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikiwemo Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda,Burundi,na Sudan Kusini lengo likiwa kuangalia mnyororo mzima wa thamani mauzo na masoko kwenye zao la korosho.

“Tunategemea washiriki wote waliohidhuria katika mafunzo haya watajadiliana vya kutosha namna gani zao hili la Korosho changamoto zinalolikabili na kupatiwa ufumbuzi kuanzia mashambani hadi masokoni “amesema Profesa.

Naye Mwakilishi kutoka Bodi ya Korosho Tanzania Dkt Rashidi Tamatama ameshukuru Tanzania kuchaguliwa kuwa nchi mwenyeji wa Mafunzo hayo kwa mara ya kwanza katika ukanda wa Mashariki na kusini mwa Afrika ambapo washiriki 75 kutoka nchi 9 kwenye ukanda huo waliohidhuria

“Tanzania ndiyo nchi inayoongoza katika uzalishaji wa zao hili ambapo Mlmwaka uliopita 2023/2024 tumezalisha tani laki tano ushirini na nane elfu kwa mara ya kwanza huko nyuma tulikuwa tukizalisha chini ya hapo” amesema Dk Tamatama.

Hata hivyo Dk Tamatama kuongezeka kwa uzalishaliji kiasi kikubwa wanaishukiru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwani izalishaji huo uliongoza kutokana na ruzuku iliyotolewa kwa wakulima na mwaka ujao 2025/2026 wamepewa lengo wazalishe tani laki saba na ifikapo 2030 uzalishaji wa zao la korosho Tanzania ifikie tani million moja.