Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,Dar es Salaam

WADAU mbalimbali na watumiaji wa huduma za bandari wameridhishwa na ubora wa huduma sambamba na utendaji kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) wakisema mamlaka imefanikiwa kukidhi matarajio ya wateja wake pamoja kuyafikia malengo iliyojiwekea.

Wakizungumza katika kilele cha wiki ya huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam jana, Mdau Hassini Norana ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam.

“Huduma za bandari zimeimarika sana sambamba na kuwepo kwa ufanisi mkubwa. Ninaipongeza TPA kwa kufanyanya maboresho makubwa,” alisema Norana na kuitaka TPA kuendelea kuzitangaza bandari zake.

Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es salaam Bw. Abed Gallus Abed akimkabidhi zawadi moja kati ya wadau wa TPA kutoka Makampuni ya Bakhresa Group Limited katika kilele cha wiki ya huduma ya wateja iliyo fanyika katika ofisi za TPA Dar es salaam kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano TPA Dkt. George Fasha.

Naye Mdau wa kutoka Bandari Kavu, Deogratius Chacha alipongeza ufanisi na utendaji uliopo kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kuipongeza Menejimenti ya Mamlaka hiyo kwa maboresho makubwa.

“Uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye Bandari ya Dar es Salaam na zile zilizopo kwenye maziwa ni Ushahidi tosha kuwa TPA imejipanga vizuri kuleta mageuzi makubwa kwenye bandari zake,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Dkt. George Fasha aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu kwenye hafla hiyo ya kilele, Plasduce Mbossa amewashukuru wadau na watumiaji wote wa bandari kwa kuendelea kuiamini na kutumia bandari zilizopo hapa nchini.

“Nikiri kuwa TPA tunauthamini sana mchango wenu kwani ni moja ya chachu inayofanikisha maendeleo ya mamlaka bna taifa kwa ujumla wake,” alisema na kuongeza kuwa, TPA imefanya maboresho makubwa nay a kisasa katika bandari zote.

Viongozi wa idara tofauti kutoka TPA (mstari wa mbele) wakiwa kwenye picha ya pamoja na miongoni mwa wafanyakazi waliopewa zawadi kwa mchango wanaoutoa katika kuhudumia wateja wao katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya huduma ya wateja iliyo fanyika katika ofisi za TPA Dar es salaam.

Dkt. Fasha alisema TPA kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 imeweza kuhudumia meli 4,487 na zilikuwa na jumla ya shehena Milioni 27.6 ambapo katika shehena hiyo makasha yalikuwa Milioni 1.1 na kuhudumiwa katika ‘terminal’ zote mbili sambamba na Bandari za Tanga na Mtwara.

“Pamoja hayo Mamlaka bado imeelekeza juhudi zake katika kuboresha miundombinu ya bandari zote ili kukidhi mahitaji ya soko linalobadilika na kukua kwa kasi huku likiwa na ushindani mkubwa toka bandari shindani,” alisema.

Dk. Fasha alisema, bado maboresho mbalimbali yanaendelea ikiwemo kujenga gati la mita 450 kwenye Bandari ya Tanga kwa jumla ya gharama ya Bilioni 429.1 na kuondoa tatizo la ‘double handling’ na pia kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es salaam Bw. Abed Gallus Abed akiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano TPA Dkt. George Fasha wakikata keki katika kilele cha wiki ya huduma ya wateja iliyo fanyika katika ofisi za TPA Dar es salaam.

Pia, alibainisha kwa wateja kuwa TPA ina mipango na mikakati kabambe ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kuhifadhi mafuta ili kupunguza muda wa kuhudumia meli nangani kutoka siku 8 hadi 10 mpaka kufika siku tatu kwa meli zenye ujazo wa 150,000 DWT na kupunguza gharama za ucheleweshaji wa meli.

“Kuanza ujenzi Gati namba 12 hadi 15 katika Bandari ya Dar es Salaam ilikukabiliana na uhaba na Magatii li Kwenda sambamba na ongezeko la meli na shehena. Gati hizo zilikuwa na uwezo wa kuhudumia makasha 1,350,000 kwa mwaka sawa na kujenga tani Milioni 31.05,” aliongeza.