Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia,Dodoma

KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua kiwango cha Elimu nchini,Umoja wa wanafunzi waliosoma Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) umezindua Mbio za Shycom Alumni Marathon zitakazo jumuisha kilometa 5, 10 na 21 ambazo zitaenda kufanyika kwa mara ya kwanza Septemba 21 mwaka huu.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mratibu wa kamati ya maandalizi Arnold Bweichum amesema lengo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule ya Sekondari Shycom iliyopo Mkoani
Shinyanga na kwamba mbio hizo zitahusisha kuibua vipaji vya watoto ambao watakuja kuwa na mchango mkubwa kwenye mchezo wa riadha nchini.

Amesema, “Tunaimani mbio hizo zinakwenda kuibua vipaji kwani makundi malimbali yatashiriki mbio hizo bila kusahau wanafunzi wanaosoma chuoni hapo na waliomaliza chuoni hapo, ” Amesema Bweichum. .

Bweichum ameongeza kuwa, ” Shycom imetoa mazao mengi, wengi wao ni viongozi wakubwa katika Serikali ya Tanzania hivyo katika mbio hizo tunakwenda kurudisha shukrani katika shule yetu kwa kusaidia pale panapo stahili lakini pia michezo ni afya, ajira hivyo tunategemea mazuri kupitia mbio hizi, ” Amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Riadha Mkoa wa Shinyanga Reuben Shampamila amesema lengo ya mbio hizo ni kufanya hamasa, umoja na mshikamano kwa wanafunzi wa Shycom kwani ni ukweli kwamba Shycom ilikuwa kumbilio la kuwajenga vijana kuwa viongozi bora.

” Tumeona tusiiachie Serikali peke, tutashikamana kuinua elimu nchini, kupitia mbio hizi tunakwenda kuboresha miundombinu ili wanafunzi waliopo na watakokuja kuweza kusoma sehemu yenye mazingira salama ,”amesisitiza

Ametaja Ada za mbio hizo kuwa ni pamoja na mshiriki anatakiwa kulipa shilingi 35000 ambapo shilingi 30000 vitaghalamia vifaa vya marathon na shilingi 5000 itaenda shuleni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati unaohitajika.

Naye Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CIG ) Charles Kichele akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliomaliza chuo cha Ulimu Shinyanga amesema wanatakiwa kurudisha shukrani katika shule yao kwani bila SHYCOM pengine wasinge kuwa viongozi wakubwa.

” Turudishe shukrani kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadae kupitia mbio hizi tunakwenda kufanya jambo kubwa na laki history, ” Amesema

Aidha ametoa wito kwa wale wote waliomaliza Chuoni hapo kuungana kwa pamoja kuchangia na kusaidia shule hiyo kwani muda wa kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa upo wakutisha.

Please follow and like us:
Pin Share