Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Simiyu
Wachimbaji wadogo wawili katika mgodi wa dhahabu Ikanabushu namba mbili ulioko katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wamekufa baada ya kufukiwa na shimo lililoporomoka wakiendelea na uchimbaji. Tukio hilo ni la usiku wa kuamkia Januari 15, 2025 saa 10 alfajiri.
Mashuhuda wanasema gema la shimo hilo liliporomoka na kuwafukia. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mtitu alithibitisha tukio hilo, alisema wachimbaji hao walivamia mashimo hayo na kuingia ndani kinyemela.
Alisema tukio hilo limesababisha vifo vya wachimbaji wawili ambao ni Mbesa Mayenga (30) mkazi wa Kijiji cha Gilya wilayani Bariadi na Yombo Yanga (32) mkazi wa Kijiji cha Dutwa huku Mayenge Zegezege akijeruhiwa.
Mtitu amesema chanzo ni uchimbaji holela usiofuata kanuni za uchimbaji madini ulio salama. Amesema wachimbaji hao walivamia licha ya awali kukatazwa.
“Wachimbaji hawa walivamia majira ya usiku na kuingia ndani ya mashimo hayo, mashimo hayo yalikuwa yamezuiliwa kutokana na kutokuwa salama, lakini wao wakaingia na yakatokea mad hara hayo,” amesema Mtitu.
Kamanda Mtitu ametoa wito kwa wamiliki wote wa mashimo kwenye mgodi, kuhakikisha wanafuata kanuni zote za uchim baji ulio salama kwa kukarabati mashimo ambayo yako kwenye hatari ya kuporomoka. Wakizungumza na waandi shi wa habari waliofika kwenye tukio hilo jana, wachimbaji wadogo walisema kuwa chanzo ni uchimbaji holela usiozingatia kanuni za usalama.
Wamesema kuwa viongozi wa mgodi walishindwa kuchukua hatua za kiusalama kwa wachimbaji hao. Mmoja wa wachimbaji hao, Dickson Julius amesema wasimamizi wa mgodi walijua kuwa mashimo hayo hayako salama baada ya kukaguliwa, lakini ha wakuwaambia wachimbaji hao.
Mchimbaji mwingine, Malimi Agustine amesema wakati wachimbaji hao wakiendelea na uchimbaji ndani ya mashimo hayo, gema moja la mashimo hayo liliporomoka.