DIRISHA dogo la usajili limefungwa rasmi Januari 16, 2024 huku tukiwashuhudia vigogo Simba wakisajili mashine mpya na kuwaacha baadhi ya wachezaji wale wa kimataifa na kitaifa kwa maana ya wachezaji wa ndani.

Simba ilifikisha idadi ya wachezaji 15 wakigeni jambo ambalo lilipelekea kupunguza wachezaji watatu ili wasalie wachezaji 12 wakigeni.

Hiyo inatokana na Simba kuongeza wachezaji wapya watatu wa kimaitaifa kupitia dirisha hili dogo la usajili ambao ni Babacar Sarr ambaye ni kiungo wa kati, Michael Fredy ni mshambuliaji wa kati na ,Pah omary Jobe ambaye ni winga wa pembeni.

Wakati huo huo, Simba imewaacha Moses Phiri, Jean Baleke na Aubin Kramo ambaye yeye ametolewa kwenye usajili kulingana na majeraha aliyonayo.

Wachezaji wengine wale wa ndani ambao Simba imeweza kuwaacha ni Jimmyson Mwinuke, Shabani Chilunda, Nassoro Kapama na Mohamed Mussa.

WALIOINGIA

BABACAR SARR

Huyu hucheza kama kiungo wa kati kwa maana ya namba 6 na 8, huweza kucheza kama kiungo mkabaji lakini akiwa na sifa kubwa ya kuchezesha timu, sababu kubwa ya Simba kumsajili kiungo huyu ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa anakwenda kumsaidia ngoma na Kanoute kwenye eno hilo.

PAH OMAR JOB

Huyu anatumia mguu wa kushoto ni raia wa Gambia ambaye anamudu vyema kucheza kama winga au pia kama mshambuliaji wa kati, anauwezo mkubwa wa kukimbia na mpira lakini pia uwezo mzuri wa kufunga mabao.

Simba wamemleta winga huyu mwenye uwezo pia wa kucheza kama mshambuliaji  ambaye amechukuwa nafasi ya Moses Phiri ambaye ameshatolewa kwa mkopo kwenda katika timu ya Power Dynamos. 

FREDY MICHAEL KOUABLAN

Huyu ni mshambuliaji wa kati raia wa Ivory Coast ambaye ametoka kukipiga katika ligi ya Zambia ambapo huko alipotoka alikuwa ni kinara wa ligi hiyo akiwa amefunga jumla ya mabao 14.

Huyu amekuja kuchukuwa nafasi ya Jean Baleke ambaye amekatwa rasmi na benchi la ufundi la timu hiyo. Sababu kubwa ya Beleke kuachwa inatokana na mapendekezo ya mwalimu Benchikha ambaye aliomba uongozi kutafutiwa mshambuliaji mwingine badala ya Baleke.

Mshambuliaji huyo ana sifa kubwa ya kufunga mipira ya kichwa kutokana na kimo chake kikubwa lakini pia ana uwezo mkubwa wa kukaa na mpira tofauti na ilivyokuwa kwa Jean Baleke ambaye pia alikuwa na kimo cha wastani.

Jean Baleke

KIKOSI KITAKAVYOKUWA

1.Ayoub Lakred 2.Shomari Kapombe 3.Mohammed Hussein. 4.Che Malone Fonde 5.Inonga Baka 6.Babacar Sarr 7.Pah Jobe 8.Fabrice Ngoma 9.Fredy Michael Kouablan 10.Saido Ntibazonkiza 11.Kibu Dennis