Sina sababu yoyote ya kuwavunjia heshima wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lakini katika enzi hizi za ukweli na uwazi sioni, sababu ya kusita kuzungumzia masuala nyeti kwa ukweli na uwazi. Lengo langu ni kuwaomba waone ugumu wa uchaguzi wa mwaka 2015.

Nikitaka kusema kweli kama ningetakiwa nizitaje kasoro za wabunge wa CCM wanapokuwa bungeni ningezitaja tatu.

 

Kwanza, wabunge wa CCM wameshindwa kwenda na wakati. Pili, wabunge wa CCM ama wamesahau, au hawajui kuwa wametumwa bungeni na wananchi kwenda kutetea maslahi ya watu waliowachagua.

 

Wabunge wa CCM wameshindwa kwenda na wakati. Kwa hiyo wameshindwa pia kusoma alama za nyakati, sasa wamekaa kutumia wingi wao kupambana na hoja zinazoletwa na wabunge wa upinzani, ambazo zinagusa wananchi na wanaziunga mkono.

 

Katika mazingira hayo, wabunge wa CCM wanajiweka mbali na wananchi kila uchao huku wabunge wa upinzani wakitumia mwanya huo kujiweka karibu zaidi na wananchi. Je, ukifika uchaguzi wowote wananchi watachagua wagombea walio mbali nao au walio karibu nao?

 

Wabunge wa CCM ama wamesahau, au hawajui kuwa wamechaguliwa na wananchi? Wanachoona wao ni kwamba wamechaguliwa na chama chao, kumbe majina yao yaliteuliwa tu na chama chao yakapitishwa na wananchi.

 

Basi wabunge wa CCM wamechaguliwa kuwa waaminifu kwa chama chao ili wateuliwe tena kuwa wagombea katika chaguzi zijazo. Kumbe majina yao yatapitishwa na chama chao lakini wananchi watachagua wagombea wa kambi ya upinzani na wa CCM wanaoonekana kuwa waaminifu kwa wananchi.

 

Wabunge wa walizingatie hilo. Wanaweza kutumia wingi wao bungeni kuwashinda wabunge wa upinzani katikati ya ushabiki wa kisiasa, lakini hawatawashinda majimboni.

 

Wabunge wa CCM ama wamesahau, au hawajui kuwa wametumwa bungeni na wananchi kwenda kutetea maslahi ya waliowachagua. Sasa wamewageuka wananchi, wamekaa bungeni kulinda Serikali badala ya kufanya kazi yao ya kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma unaofanywa na Serikali na vyombo vyake – wamekaa bungeni kupangua hoja za msingi za elimu, maji, ajira na nyinginezo zinazoletwa na wabunge wa kambi ya upinzani badala ya kuziunga mkono.

 

Ni wazi kwamba wabunge wa CCM wamekaa bungeni kufunika mijadala ya maendeleo na yenye maslahi kwa wananchi waliowachagua. Hapana shaka lengo la wabunge wa CCM ni kuwaondolea umaarufu wabunge wa kambi ya upinzani. Kumbe wanawaongezea umaarufu mbele ya wananchi ambao wanawaona kwamba wao ndiyo watetezi wao wa kuwategemea.

 

Wakati huohuo, kuna ukweli usiopingika kwamba wabunge wengi wa CCM hawatembelei watu wao majimboni. Wamejigeuza kuwa walowezi wa mijini, kwa hiyo hawajui kinachoendelea majimboni  kwao wala matatizo ya watu wao. Wanachosubiri ni kwenda bungeni kupata posho tu, huku wengi wao wakiwa hawaonekani kwenye vikao vya Bunge.

 

Katika mazingira hayo ya kwenda bungeni bila kujua kinachoendelea majimboni kwao, wabunge wa CCM wamejikuta hawana jipya la kuzungumzia bungeni. Wanabaki kusubiri hoja za wabunge wa upinzani wazipangue. Kama huko si kushindwa kufanya kazi waliyotumwa na watu wao wa majimboni mimi sijui ni kitu gani.

 

Watu wamesema; “Samaki mmoja akioza wote huoza.” Katika suala hili la wabunge  wa CCM methali hii haina nafasi. Wananchi wanajua fika kuwa wapo wabunge wachache wa CCM wanaowawakilisha kikamilifu watu wao wa majimboni, miongoni mwao wamo akina Deo Filikunjombe (Ludewa), Kangi Lugola,(Mwibara), Luhanga Mpina (Kisesa), James Lembeli (Kahama), Ezekiel Maige (Msalala) na Rama Makani (Tunduru).

 

Mbele ya wabunge wenzao wa CCM hapana shaka wabunge hao wanaonekana wanakisaliti chama, kwa hiyo inaweza kufanyika juhudi au mizengwe ya kuwafukuza kwenye chama. Wakifukuzwa wasisite kujiunga na vyama vya upinzani, kwa vyovyote watachaguliwa na wananchi. Hawa ni wabunge jasiri walioamua kuwa waaminifu kwa watu wao waliowapeleka bungeni.

 

Wakati huo huo, kuna hizi tetesi za kutungwa sheria ya kupambana na uchochezi, hapana shaka lengo la sheria hiyo ni kuwaziba midomo wapinzani. Tumeshindwa kutofautisha ukweli na uchochezi.

 

Chukua kwa mfano, Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, anaposema kwamba katika suala la udini Serikali inapaswa kulaumiwa kwa sababu ndiyo chanzo cha chokochoko za udini ambazo matokeo yake yamekuwa vitendo vya kigaidi. Wananchi wanajua kuwa huo ni ukweli na wala si uchochezi.

 

Si kweli kwamba mihadhara ya kuchochea chuki imeachwa iendeshwe na Waislamu kwa muda mrefu bila kuchukuliwa hatua? Si kweli kwamba CD za kuhamasisha mauaji ya viongozi wa dini ya Kikristo ziliachwa zisambazwe na sheikh mmoja wa Mwanza nchi nzima bila kuchukuliwa hatua? Na sasa walitaka kumuua Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini, Francisco Montecillo Padilla, tukio ambalo limeifedhehesha sana Tanzania.

 

Halafu wapinzani wakisema udini umeasisiwa au umepaliliwa Ikulu ni uchochezi? Huu si ukweli? Je, kwa mfano, kulikuwa na sababu gani ya kutosha Ikulu kuteua Jaji Mkuu Mwislamu, Jaji kiongozi Mwislamu, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mwislamu na kadhalika?

 

Je, katika nafasi hizo zote hakuna hata moja ambayo ingeweza kushikwa na Mkristo? Maana hali hii imetoa nafasi kwa Wakristo kudai kwamba hali ya mambo katika Tanzania ya leo ni mbaya kwa sababu Waislamu wameshindwa kuendesha nchi.

 

Kwa upande huo wa udini ukweli ni kwamba Serikali imewadekeza mno Waislamu. Wameendelea kuutukana Ukristo kwa muda mrefu bila kuchukuliwa hatua, gazeti lao moja limeendelea kujikita kwenye uchochezi wa kidini. Na kule Mwanza sheikh mmoja alipewa nafasi ya kusambaza nchi nzima CD zilizohamasisha Waislamu kuua viongozi wa Makanisa.

 

Tumesikia viongozi wakipiga kelele zinazotaka Waislamu na Wakristo wavumiliane kana kwamba nao Wakristo ni wachochezi. Wachochezi ni Waislamu na hao ndiyo wanaoendesha mikutano ya Injili ambayo inazungumzia dini yao tu. Basi ni Waislamu wa kunyooshewa vidole ndiyo wanaoendesha vitendo vya chuki na ugaidi duniani kote. Na sasa wamepewa nafasi Tanzania.

 

Mbunge Jemes Mbatia amedai kwa haki kabisa kuwa mihadhara ya dini ipigwe marufuku moja kwa moja, lakini Serikali iliyokaa kuwadekeza Waislamu inadai itadhibiti mihadhara ya dini, wanachojua wananchi ni kwamba Serikali haijawahi kudhibiti jambo lolote kwa ufanisi, kwa hiyo mihadhara itaendelea kupandikiza chuki za kidini Tanzania, na Waislamu na Wakristo wataendelea kupigiwa kelele za kutakiwa wavumiliane.

 

Kinachosisitizwa hapa ni umuhimu wa Serikali na wabunge wa CCM kutopuuzia kila hoja na kila ushauri unaotolewa na wabunge wa upinzani na wabunge wachache wa CCM wanaosoma alama za nyakati.

 

Wananchi wanajua kuwa wabunge hawa ndiyo wanaotetea maslahi ya taifa na maslahi ya watu waliowachagua. Wabunge waliokaa bungeni kuitetea Serikali na chama chao wawe na hakika kwamba hawatarejeshwa bungeni mwaka 2015. Anayebisha asubiri.