WATU wasiopungua 12 wameauwa katika mashambulizi mapya ya waasi wa kundi la ADF lenye mafungamno na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS.

Watu wasiopungua 12 wameauwa katika mashambulizi mapya ya waasi wa kundi la ADF lenye mafungamno na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mashambulizi hayo yanatokea baada ya mkururo wa mashambulizi mengine ya ADF katika kipindi cha Krismasi yaliyowaua watu 21 katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Maafisa wa eneo hilo wamesema mashambulizi hayo yametokea usiku wa kuamkia Jumatano na yalilenga maeneo mawili katika jimbo moja. Afisa mmoja Samuel Kagheni, amelieleza shirika la habari la AFP kwamba waasi hao waliwaua watu wanane katika kijiji cha Bilendu. Watu wengine wanne waliuawa katika kijiji cha Mangoya, huku waasi wakichoma nyumba katika maeneo yote mawili.

Mwaka 2019 kundi la waasi la ADF lilitangaza utii kwa kundi la IS.